Kuna ugonjwa wa wasiwasi (hofu)?

Hii hali ilishawahi kunitokea Na niliwekewa mpk drip la maji ili kushusha presha....Huyo hali ilinijia ghafla tu Na nilipimwa cha ajabu hakuna ugonjwa wowote uloonekana ila ilidumu kama wiki 2 hv...yan wasiwasi mtindo mmoja na muda wote unawaza kifo tu..Mwisho madaktari waliniuliza vp una tatizo lolote la kifamilia au umepata Habari mbaya? nikawambia Hapana sin Habari yyte mbaya Na maisha ninayoishi ya kawaida tu Na sina msongo wowote.Hali Hii ilidumu kama wiki 2 HV Na kila nikijaribu kuuliza watu hakuna mwenyewe jibu la kunituliza ila kila ninapoenda msikitini kuswali nikishamaliza Ndo Kuna afadhali naipata then hali inarudi tena...ila nilijitahidi sana Na swala mwisho ikapotea mpk Leo Ni mwaka wa 4 sijaona tena.Hapa karibuni nilikuwa Na mamamkwe wangu ktk maongezi aliniuliza vp ile hali inakusumbua tena? nikamwambia Hapana Nina muda mrefu sijaiona tena,akanambia kuwa ile hali SAA zingine huwa inawakuta wanaume ambao wake zao sana mimba change,yaani mke wako akiwa Na mimba changa Yale mahangaiko mwanamke mjazito anayoyapa pindi mimba Ikiwa changa mahangaiko Yale huhamia kwako mwanaume....Na Hili la wasiwasi Ndo huwa linachukua nafasi kubwa.Sasa nikajaribu kukumbuka Ni kweli kipindi hali ile inanitikea mke wangu alikuwa Na ujauzito wa kama mwezi 1 Na cha ajabu wakati Mimi nahangaika Na ile wasiwasi yeye alikuwa kama vile hana mimba Na alikuwa kabisa hajihisi chochote so hebu jaribu kuchunguza hilo kwanza na kufanya sana sala...maana sometimes Mungu huwa anakuzindua urudi katika ibada kwa sababu sehemu kubwa ya huo wasiwasi Ni kuwaza waza kifo muda wote,Ila usiogope Ni hali ya kawaida sana Na Mimi imenitokea kama nilivyokwambia....ila kama Ni Muislam jitahidi kuswali sana hiyo hali itapotea ila usiache ibada na kumtaja sana Mungu Ni muhimu sana Na itakupa Amani ya moyo Na utulivu wa ajabu.
 
Mkuu mm hii hali inedumu kwa mda toka mwezi wa saba mwaka Jana!!!
Lkn pia nilikuwa nasumbuliwa na vidonda vya tumbo ambavyo kwa sasa kuna asilimia flani naona vimepungua sana!!!
Kuna kipindi nilikuwa na mawazo sana mwaka 2015 karibia mwaka mzima na kidogo
 
Daaaaaah mkuu damu yangu kwixha kwa hyo lugha
 
mkuu na mimi nna tatizo hilo mkuu,jibu la hapa pengine na mimi litanisaidia
 
jamaa alizingua nini?
 
Kiongozi kwanza pole kwa tatizo uliyokuwa nalo,hili tatizo wanalo watu wengi na mwanzoni lilipokupata ulidhani ni ugonjwa ambao unao pekee yako ila unapata faraja kubwa kujitokeza kwa wana jf wengine kukwambia nao wana tatizo kama la kwako.
Huu ugonjwa kwa hapa kwetu wataalam wa tiba bado wanahangaika nao (mimi ni muhanga pia) hawana tiba ya kueleweka. Hivyo zidi kupata ushauri kwa waliopata maradhi haya na utapata nafuu. Mimi uliniweka chini mwaka mzima namshukuru Mwenyezi Mungu naendelea vizuri Alhamdulillahi. Nilihangaika sana kwenye tiba kilichonisaidia zaidi nilipokua naongea na baadhi ya jamaa zangu wakaniambia nawao pia wanatatizo hilo wengi walipata nafuu kwa kumuomba Mungu na nashukuru nimedumu katika ibada imenisaidia sana.
Angalizo usiende kwa waganga wa tiba zetu za jadi au asili utaliwa pesa zako.
 
Reactions: GUI
Asante mdau
 
mkuu na mimi nna tatizo hilo mkuu,jibu la hapa pengine na mimi litanisaidia
Ngoja tuendelee kuwasubiri ndugu zetu walio wahi kupitia na wakapona huenda watatusaidia
 
Nimeona maswali ni mengi juu ya tiba ya ugonjwa huu wa Hofu.

Kwanza mambo yakuepuka kabla sijakushauri tiba ni

Vitu vyenye sukari nyingi, hivi vitaongeza kiwango cha sukari mwilini na kupelekea sukari kwenye damu kuongezeka na kukuongezea tatizo

Kahawa, drinks energy na vileo sio vyote, (you can take red wines) hivi vinywaji huongeza uongezeko la msukumo wa damu (Blood pressure) hivyo kufanya mapigo ya moyo kuwa kasi na kuzidi kukufanya uogope.

Tiba:
Hofu ni Ugonjwa wa Kisaikolojia, yaani ni ugonjwa wa matukio au mambo yakufikiria, yasiyo halisi au halisi yasiyokuwa dhahiri au usibitisho.

Dawa za ugonjwa huu ni kuutibu kisaikolojia na sio kikemia (kutumia madawa ya hospitalini) Dawa za Hospitalini zinatibua utaratibu wa mfumo wa mwili na usipopona kwa muda amabao mawazo yako yanakutuma unaweza kuapata matatizo zaidi. Pia dawa hizi zinaweza kusababisha chemikali (homone) zakuzuia woga kuzalishwa kwa wingi kuliko uhitaji wa mwili na tatizo likasalia pale pale. SISEMI DAWA ZA HOSPITALI NI MBAYA NA WALA SIKWAMBII UENDE KWA MGANDMGA, laah hasha, ninachomaanisha ni kwamba zina ufanisi mdogo kwa ugonjwa kama huu.

UFANYE NINI KUONDOKANA NA TATIZO HILI?

Mosi, kula vyakula vya asili vyenye virutubisho vya vitamini B kama vile vyakula vya majini hasa hasa samaki (wakuchemsha ndio wazuri zaidi vitamini vinabaki katika ubora wake), spinachi, Ndizi mbivu, viazi mviringo n.k

Kula vyakula vyenye Kalsiamu(Calcium) na Sodiamu (Sodium) kwa wingi kama vike parachichi, baadhi ya mboga za majani, minofu ya mifupa, au mifupa iliyosagwa, saladi, na zabibu.

Pili, na katika UMUHIMU:
Tambua chanzo cha tatizo lako, kama ni Ugonjwa utafutie tiba, kama unahisi ni ugonjwa usiopona, amini hautaishi milele na ipo siku utakufa lakini siku yenyewe iko mbali sana licha hali uliyonayo.
Amini wapo wengi walioishi na ugonjwa kama wako kwa miaka mingi sana bila kufa wala kushindwa kufanya shughuli zao, amua leo.

Kama ni hofu ya matatizo ya kifamilia/ukoo mf. Uchawi, Usiogope mfanye mnayedhani mchawi kuwa rafiki, usimwogope (hatakuloga kirahisi), Usiende kwa waganga, watakuchanja mwili mzima na hutapona.
Mwombe sana Mungu, mwombe toba kwaajili yako, mwombe akuweke huru na vifungo vya familia/ukoo wenu,.

Jitenge na mambo yanayokuongezea hofu.

Jitahidi usiku ulale kabla ya saa nne usiku, ili kuipa akili muda wakutosha wakupumzika baada ya quarrels nyingi za mchana, mwili nao upate ahueni, pia wahi kuamka na ufanye mazoezi laini kama kuruka kamba n.k

Pendelea kulala kwa mgongo muda mchache kabla yakuzama usingizini huku ukipumua kwa kasi, yaani unavuta hewa nyingi ndani kisha unatoa hivyo kwa nguvu (HII NI DAWA YA WATU WENYE HOFU ILIYOPITILIZA PIA WAGONJWA WA PRESHA NA MOYO) Hii hufanya ubongo kupata hewa na kurelaxy, na akili yako badala yakufikiria unachokihofia, itawaza namna unavyovuta hewa ndani na kuirudisha, pia itafanya mishipa na misuli ya moyo (cardiac muscles) kutanuka na kuacha moyo nafasi yakutosha ili usipatwe na shambulizi la moyo.

Penda kusoma storibza kufurahisha, au kutazama runingani.

Kama Mke/Mume(unayemwamini na asiye chanzo cha tatizo lako) get a sex once/twice per week. Ngono salama husaidia kutuliza akili na kuketa raha moyoni(ikiwa umefanya kwa halali, hujadokoa mwanafunzi au mke wa mtu au mtu unayemhofia kuwa na VVU)

Ukihisi hofu, kunywa maji mengi ya baridi(yasiwe yabaridi sana yakukushinda kunywa mfululizo), Ikiwezekana Oga kwa maji ya baridi taratibu bila haraka huku ukijimwagia kichwani, kama una shower itakuwa nzuri zaidi (ukioga maji ya baridi itakufanya mwili na akili kurelax)

Jitahidi unapoamka au mchana unapokuwa mwenyewe, jichetue ucheke kama uliyechekeshwa na kitu.

Ukiwa nyumbani mchana pata walau dk 45 au saa moja la kulala.

Jichanganye na watu, fanya kitu unachopenda ili mradi kisiwe kibaya au chenye kukufanya baadaye ujutie, mf. Kutumia pesa kwaajili ya starehe, zikiisha utapata msongo wa mawazo.

Jifunze kusamehe na kutokuona sababu ya kutunza kinyongo au kuwa na maeazo yakulipiza kisasi, hii itakuondolea stress. Mpende ambaye hukumpenda siku za nyuma, hii itasaidia kuleta suluhu.

Mwisho kabisa Kuwa mtu wa Ibada, haijalishi ni dini gani, Jifunze kuongea na Mungu sana, usiku na mchana, ukizinduka usingizini usiku mwambie Mungu asante, omba dua njema kwako na kisha endelea kulala.

Hakuna magumu hapa duniani yaso mwisho. Jipe moyo.
 
Asante dogo, japo inatesa sana maana kichwa kikivurugika kila kitu mwilini hakikai sawa
 

Inaitwa "Generalized Anxiety Disorder"

Ripoti hospital ya Muhimbili kuna Madaktari na wanasaikolojia watakusaidia kwa ufanisi
 
Ndugu fuata ushauri huu utakukusaidia
1. Fanya mazoezi ya kuongeza mapigo ya moyo mfano kukimbia au nenda gym Mara 5 kwa week ( itakuongezea furaha na kujiamini)
2. Jifunze Ku meditate au yoga na ufanye kila siku
3. Anza kupumulia tumboni na sio kifuani
. na muda wwte utakao pata woga vuta pumz kwa Tumbo na u hold kwa sec 5 na utoe kwa mdomo kwa sec 8 fanya hadi usikie woga umeisha
4. Waza mawazo chanya siku zote.

Unipe taarifa unaendeleaje
 
Asante mkuu
 
Inaitwa "Generalized Anxiety Disorder"

Ripoti hospital ya Muhimbili kuna Madaktari na wanasaikolojia watakusaidia kwa ufanisi
Asante mdau
 
Mkuu hilo tatizo linakuwa solved, its just a matter of reprogramming tu kwenye suala zima la ki mental activities, nishakutana na hizo case nyingi mno...
Mie pia niliwahi kuwa attacked ila it was a side effects wa mafunzo.. mie nilifanyia practicle ili kujua undani na mwishoni nikajua namna ya kulitatua..niligundua mengi mno behind hilo tatizo... kwa sasa naweza kukupa ushauri wa fasta ni kwamba I check hio attitude yako .. ifanyie overalls.. kwa kuifanyia utafiti... then turn it to positive kwa chochote kile...

Mambo mengine ni umpate mtu akufanyie sessions ambayo baadae itakupa mwangaza na namna vitu vinavyo tokea na pia utaziona fursa through hio sessions
 
Ugonjwa mbaya sana huo unapelekea moyo kwenda speed jitaidi kujishulisha na vitu vinavyo kupa furaha utapona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…