A
Anonymous
Guest
Ninaomba kuwasilisha kero kuhusu uhaba mkubwa wa walimu wa somo la Literature katika shule nyingi za serikali kwa ngazi ya kidato cha tano na sita.
Serikali ilianzisha kombi mpya za masomo, ikiwemo HGLI na HKLI mwaka 2023, lakini hadi sasa hakuna ajira ya kutosha ya walimu wa somo la Literature waliopangwa kufundisha katika shule hizo. Hali hii imeleta changamoto kubwa kwa wanafunzi wanaochukua kombi hizo.
Kwa sasa, kuna shule kadhaa zilizoathirika na uhaba huu wa walimu, zikiwemo Shule ya Sekondari Dakama, Kigwe na Nsumba, ambapo wanafunzi wanakosa mwongozo sahihi katika somo hilo muhimu.
Kutokana na hali hii, wanafunzi wanapata ugumu katika maandalizi ya mitihani yao, jambo ambalo linaweza kuathiri moja kwa moja matokeo yao ya kitaaluma.
Tunaomba mamlaka husika kuingilia kati kwa haraka ili kuhakikisha walimu wa kutosha wa somo la Literature wanaajiriwa na kupangiwa katika shule husika, ili kulinda ubora wa elimu na mustakabali wa wanafunzi.