Kuna uhaba wa mafundi ujenzi tangu Desemba 2024. Chanzo ni nini?

Kuna uhaba wa mafundi ujenzi tangu Desemba 2024. Chanzo ni nini?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Tangu December 2024 hadi sasa January 2025 nimebaini uhaba mkali sana wa maafundi ujenzi (Uwashi, nk.) .., uhaba ni mkali mno! Mafundi Uwashi ni wa kugombania hasa jijini Dar. Chanzo ni nini?

At the same time kuna wimbi kubwa la vijana naliona likishinda kucheza kamari kwenye mabanda mbali mbali ya mpira na vijiwe vya kamari. Je, tatizo ni ubovu wa mfuno wa elimu kwa kutojumuisha ufundi stadi wenye high demand na mchango mkubwa katika ujenzi na ustwei wa taifa?

Mafundi ujenzi wa kueleweka karibu wote wapo Kariakoo, huku mtaani mafundi wengi wamebaki ni wanywa visungura vile vikali, ukimpa kazi ukuta unapinda pinda kama mti wa mbuyu.

Kule Ujerumani hurusiwi kusime degree ya aiana yeyote ile kama huna cheti cha ufaulu wa ufundi stadi wa aina yeyote, hata kama unataka kuchukua degree ya sheria, lazima kwanza usimee na kufaulu ufundi either wa umeme, Mekanika au chochote kile..
 
Kuna mafundi niliwapa kazi yangu Dodoma nimeenda nimekuta hawajaifanya, material hayapo na hela nilishawamilizia, nchi ngumu sana hii
Mimi wa kwangu nikimlipa advance ya ufundi, kapata kazi sehemu nyingine yenye maslahi makubwa kakimbia.., na hadi sasa nahangaika kutafuta fundi wa kueleweka wa permanent, hawapatikani..
 
Mi nimelala hapa nasubiria kazi itokee nikiperuzi jf taratibu. Muhimu ukifanya kazi na mimi tusainishane kwa usalama wangu na tajiri
 
Mfumo hakuna wa kuwasajili na wakutoa reference. Ingekua kuna data base yao na reference ata online, tungekua tunajua huyu ni fundi mwizi na asingekua anapata kazi
Ni kweli Kaka ,Sasa ushakuwa hivyo na tayari wamekuibia ,ndiyo maana naendelea kukuomba na kukusitiza kuwa tunawaomba tuwapige viboko iwe fundisho kwa wengine .
 
Ni kweli Kaka ,Sasa ushakuwa hivyo na tayari wamekuibia ,ndiyo maana naendelea kukuomba na kukusitiza kuwa tunawaomba tuwapige viboko iwe fundisho kwa wengine .
Huko kwenu nako ni shida, tukiwaletea wateja ni kama tumewapa dili, hakuna kinachofanyika. Si kwa ubaya, ndiyo ukweli wenyewe
 
Back
Top Bottom