Habari za wakati huu watanzania wenzangu.
Kuna makala niliweka humu juu ya uandaji wa mbolea ya samadi ya maji kwa ajili ya matumizi ya bustani na shamba kiujumla. Kulingana na watu walionitafuta kuhitaji kujua zaidi na mrejesho ninaoupata kwa walioanza kutumia hakika ninapata faraja kubwa sana.
Ukweli ni kwamba unaweza kuandaa mbolea za asili ukazitumia katika kilimo chako cha mboga mboga na hata kilimo cha nafaka na ukapata matokeo mazuri sana.
Ili mmea uweze kumea vizuri unahitaji kupata virutubisho muhimu kwa ukuaji wake na hata utiaji wa matunda. Virutubisho hivyo ni nitrogen (N) phosphorus (P) na potassium (K), (NPK) na hivi ndivyo virubisho muhimu sana kuwepo ili mmea uweze kuwa na ukuaji na uzao mzuri. Lakini ili kupata matokeo mazuri zaidi lazima pia virubisho vingine vipatikane kama Zinc, iron, calcium, magnesium, boron, manganese n.k..
Hivi virutubisho vyote vyaweza kupatika katika mbolea ya asili ambayo unaweza kuandaa nyumbani au shambani kwako. Unaweza kuandaa mbolea yako kwa kutumia kinyesi cha ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku, n.k. mkojo wa ng'ombe, mbuzi, kondoo, sungura nk.., mabaki ya mboga mboga na matunda ya sokoni, mabaki ya chakula, sukari guru au molasses au sukari, amira, maziwa na majivu.
Mbolea utakayoipata hapo itakuwa na nguvu na Huwa na matokeo chanya ya haraka zaidi
Hapa nakupa namna ya kuandaa moja ya mbolea hizo. Hapa tutajifunza kuandaa lita 20 ya mbolea ya maji na matumizi yake.
MAHITAJI
1. Ndoo moja la lita 20
2. Kinyesi cha ng'ombe kilo 2
3. Mkojo wa ng'ombe lita 2
3. Maziwa lita 1
4. Majani mabichi kilo 2
5. Majivu kikombe kimoja cha nusu lita.
6. Sukari robo kilo au molasses nusu lita.
7. Mabaki ya chakula (unga robo kilo)
8. Maji.
HATUA ZA KUFUATA.
1. Weka malighafi zote kwenye ndoo kisha koroga vizuri kwa dakika 2 mpaka 5. (hakikisha majani kabla ya kuweka kwenye mchanganyo umeyaponda vizuri na kusagika)
2. Funika mchanganyo wako katika ndoo na ruhusu hewa kutoka kupitia tundu dogo sana. Weka katika kivuli au sehemu ya baridi.
3. Unatakiwa kuukoroga kila siku kwa muda wa siku 14 na kuufunika.
Baada ya siku 14 mbolea itakuwa tayari kwa matumizi
MATUMIZI
Utachanganya cc 500 mpaka lita 1 kwa lita 15 mpaka 20 za maji kutegemea na asili ya udongo na aina ya mimea unayolima. Hii ni kwa ajili ya kunyunyiza kwenye udongo (mizizi) tu
Ukitaka kutumia kama busta (foliar spray) tumia cc 50 mpaka 100 kwa pampu ya mgongoni ya lita 15 hadi 20.
NB. Mbolea hii haina sumu yoyote wala madhara kwa mtumiaji wa mboga mboga. Pia haina harufu mbaya.
Kama umevutiwa na makala hii weka comment yako hapo chini. Pia unaweza wasiliana nami kwa namba 0621039828. Pia unaweza wasiliana nami kwa Whatsapp video call Видеозвонок WhatsApp
Karibu sana