Musundi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 1,584
- 2,613
Enzi hizo za ujana nakumbuka tukio moja lililonikuta huko kwetu nyumbani kijijini mpaka leo najiuliza na hapa nawauliza ninyi wajuvi wa mambo kama kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya jicho na pua.
Ilikuwa majira ya saa 4 hivi asubuhi nilipoingia ndani jupitia korido lenye mwanga hafifu. Ghafla nilikanyaga jembe lililoachwa njiani bila tahadhari. Hamad...! Mpini ulinipiga jicho la kushoto mpaka nikaona manyotanyota na kupata maumivu makali sana. Tokea hapo jicho halikuona tena kawaida maana kila nikijaribu kuangalia vitu niliviona viwiliviwil.
Kilichonitisha zaidi na ndio msingi wa uzi wangu huu ni kwamba mara damu ilianza kutoka puani (ndewe ya kushoto) nikalazimika kuiziba na pamba. Sababu ya maumivu makali na macho kutoona kawaida tena nililazimika kulala kwa masaa 3 hivi.
Nilipoamka damu ilishakata na macho yanaona kawaida.
Swali langu: Kwa trauma hiyo niliyoipata, kwa nini damu itoke puani na nini kilitokea jichoni mpaka kuona taswira mbilimbili?