Kuna uhusiano gani baina ya jicho na pua?

Kuna uhusiano gani baina ya jicho na pua?

Musundi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
1,584
Reaction score
2,613
Enzi hizo za ujana nakumbuka tukio moja lililonikuta huko kwetu nyumbani kijijini mpaka leo najiuliza na hapa nawauliza ninyi wajuvi wa mambo kama kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya jicho na pua.

Ilikuwa majira ya saa 4 hivi asubuhi nilipoingia ndani jupitia korido lenye mwanga hafifu. Ghafla nilikanyaga jembe lililoachwa njiani bila tahadhari. Hamad...! Mpini ulinipiga jicho la kushoto mpaka nikaona manyotanyota na kupata maumivu makali sana. Tokea hapo jicho halikuona tena kawaida maana kila nikijaribu kuangalia vitu niliviona viwiliviwil.

Kilichonitisha zaidi na ndio msingi wa uzi wangu huu ni kwamba mara damu ilianza kutoka puani (ndewe ya kushoto) nikalazimika kuiziba na pamba. Sababu ya maumivu makali na macho kutoona kawaida tena nililazimika kulala kwa masaa 3 hivi.

Nilipoamka damu ilishakata na macho yanaona kawaida.

Swali langu: Kwa trauma hiyo niliyoipata, kwa nini damu itoke puani na nini kilitokea jichoni mpaka kuona taswira mbilimbili?
 
Baada ya tukio hilo ulikwenda kutibiwa? Daktari aliyekutibu angeweza kukuelezea vizuriii sana.
 
Kwa akili ya kawaida tu..jicho na pua ni viungo vilivyo karibu sana..ss ulipogonga jicho kuna uwezekano ulipasua mishipa ya damu ya kwny pua..ndo maana ukatoka damu puani!!
 
Baada ya tukio hilo ulikwenda kutibiwa? Daktari aliyekutibu angeweza kukuelezea vizuriii sana.
Sikwenda hospitali wala sikutumia dawa yoyote. Kumbuka mazingira ya kijijini
 
Baada ya tukio hilo ulikwenda kutibiwa? Daktari aliyekutibu angeweza kukuelezea vizuriii sana.
Sikwenda hospitali wala sikutumia dawa yoyote. Kumbuka mazingira ya kijijini.
 
Kwa akili ya kawaida tu..jicho na pua ni viungo vilivyo karibu sana..ss ulipogonga jicho kuna uwezekano ulipasua mishipa ya damu ya kwny pua..ndo maana ukatoka damu puani!!
I agree na pia huenda hata puani ulipigika ila labda maumivu ya jicho yalikuwa so intense mpaka hukuweza Ku notice
 
Ngoja nisubirie jibu hapa maana pia pua ikiumizwa huwa jicho linatoa machozi automatic
 
Back
Top Bottom