Kuna uhusiano gani kati ya nyimbo na uchungu wa nafsi?

Kuna uhusiano gani kati ya nyimbo na uchungu wa nafsi?

Blue Bahari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
1,851
Reaction score
2,171
Habari za mwaka mpya wandugu. Natumai mko poa kabisa.

Nina hoja ambayo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu, kwamba inatokana na nini?

Ni hivi, je umewahi kusikiliza wimbo fulani kisha ukajikuta unaanza kupatwa uchungu wa nafsi? Namaanisha unapousikiliza wimbo fulani unajikuta ni kama unataka au kujikuta unadondosha machozi pale unapoendelea kuusikilza wimbo huo.

Nauliza hivyo kwa kuwa mimi binafsi huwa inanitokea mara nyingi pale nisikilizapo baadhi ya nyimbo, huwa najikuta napatwa na uchungu wa nafsi mpaka kufikia kutaka kumwaga (au kutoa kabisa) chozi hata kama nilikuwa katika hali ya kawaida kabisa kabla ya kusikiliza nyimbo hizo.

Je, wewe huwa hali hiyo inakutokea? Na je, halo hiyo inasababishwa na nini? Kuna uhusiano gani kati ya music na uchungu wa nafsi?

Karibuni.
 
Hii inatokea pale ambapo wimbo husika umegusa tukio lililowahi kuigusa nafsi yako yako kwa namna ya kipekee iwe ya furaha au huzuni.
 
Dhana Kuu ya Nyimbo na Uimbaji ni Hisia Ndugu na ndiyo maana kuna Nyimbo zinatuhuzunisha na kutufurahisha. Tungo zote huwa ni Hisia tupu.
 
Ni kweli nyimbo in hisia. Je, ushawahi kutoa chozi wakati ukisikiliza wimbo flani?
Kwani ni lazima ukiwa na Hisia Kali basi lazima ( yakupasa ) ulie Ndugu? Katika Binadamu ambaye Machozi yake yako mbali kabisa Kulia ni Mimi tu.
 
Mi sinaga hizo mnaita hisia.
Hisia unazo, labda kwako ni kwa kiwango kidogo. Binadamu yoyote yule lazima uwe na hisia. Kwani mkeo/demu wako ulimpata pasipo kuwa na hisia naye?
 
Mbona uhusiano upo! We unaionaje awamu hii..😂
 
Wimbo wa Bob Marley "Chances Are" huwa unanitoa machozi.

Yani hapa nimeanza kuusikiliza tu naona machozi yanaanza kunitoka. Imebidi niukatishe kabisa yani nimeshindwa kumaliza kusikiliza wote. Ni wimbo maalum ninaosikiliza kwenye misiba ya watu ninaowapenda.Bob Marley analalamika sana kuhusu huzuni katika maisha.

Ni mambo ya hisia zaidi. Dr Robert Sapolsky ameelezea kirefu sana katika kitabu chake "Behave: The Biology of Humans at Our Best and Worst"

Kuna bidada mmoja rafiki yangu alifanya Ph.D yake ya Clinical Psychology kwenye swali hili. Nitamuuliza kupata maoni ya kisomi.

Ukipata jibu nitag mkuu.
 
Back
Top Bottom