May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Natumai wengi mtakubaliana nami kuwa Duniani tupo Watu wa aina tofauti..hii imepelekea wengi wetu kuhusisha baadhi ya matendo na aina fulani ya Watu. Kwa mfano kuna aina fulani ya Watu ukimkuta anafanya shughuli fulani lazima moyo wako utashtuka kwanza na utatamani kujiridhisha ni kwa nini Dada/ Kaka au Mama/ Baba huyo yupo kwenye shughuli ile.
Iwe ni Mwanamke au Mwanaume zipo sura au muonekano ambao utaona Mtu mwingine anatumia nguvu kubwa kukuaminisha kuwa Mtu huyo ni tofauti kabisa na anavyoonekana. Mathalani utamsikia Mtu akikuaminisha jinsi fulani alivyo na roho nzuri au upendo, na kinyume chake Wapo ambao inalazimika Mtu kumuelezea namna alivyo na ukosefu wa dabu na heshima ili tu usihadaike na muonekano wake.
Kuna Mtu ukiambiwa ni Mwizi au Jambazi anayevunja nyumba za Watu usiku basi utabaki na mshangao, na Wapo ambao ukiambiwa hivyo wala hutoshtukakwa jinsi Mtu huyo anavyoonekana.