Kuna ukweli gani juu ya wapiganaji kuaminishwa risasi kugeuka maji kwenye Vita ya Majimaji?

Kuna ukweli gani juu ya wapiganaji kuaminishwa risasi kugeuka maji kwenye Vita ya Majimaji?

Unasemeje

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2021
Posts
249
Reaction score
923
Hii ni hekaya ambayo hai ingii akilini, eti watu walidanganywa risasi zitageuka maji na wakaingia mkenge, huu ni uongo, hivi mnajua mlio wa bunduki nyie?

Mimi nadhani majimaji ilikuwa ni mgomo ulio ambatana na vurugu, na baadaye wajerumani wakawatembezea kichapo wahusika, basi.

Hizo habari nyingine kwakweli mimi nadhani ni uongo na hakuna maana kuwafundisha watoto wetu, tunawafundisha kuwa waongo waongo tu, maana hata evolution of man ni uongo tu.

Vita halisi ilikuwa ile ya Tanzania na Uganda.
 
Kwahiyo umefikira mambo ya kale mpaka ukahitimisha kuwa ni uwongo?

Hebu achana na mambo ya kale anza kufikiria hawa watu wanao danganywa na manabii wa kisasa.

Mfano zumali nk au vizazi vijavyo tukija kiviambia kuwa kuna watu walikuwa wanajitoa muhanga na wenyewe watajua ni kamba kumbe ilikuwa kweli
 
Hiyo dhana na nadharia Yako ni batili. Hayo ndio mapambano sasa..maji maji is more than Idd Amin war...unapigana na rngi nyeupe yenye Kila aina ya teknolojia ya kisasa wakati huo. H
 
Hii ni hekaya ambayo hai ingii akilini, eti watu walidanganywa risasi zitageuka maji na wakaingia mkenge, huu ni uongo, hivi mnajua mlio wa bunduki nyie...
Vipi kuhusu na wale waliopigwa kiberiti na kibwetere ikiwa unaamini maji maji ni uongo
 
Vipi kuhusu na wale waliopigwa kiberiti na kibwetere ikiwa unaamini maji maji ni uongo
Huyo ndugu yetu, arudie kufikiri tena. Usimkumbushe vitu vya mbali anaweza sema alikuwa mdogo wakati yanatokea ya kibwetere.
Je hao majirani zetu Kenya walio kufa kwa kufunga msituni wa shakahola huku mchungaji akizidi kunenepa kwa sadaka zao? Au na yenyewe ni uwongo?
 
Kama pamoja na maaendeleo ya sasa, utandawazi, elimu na mitandao, bado watu wanakufa wakikanyaga mafuta ya mwamposa.
Sembuse watu enzi hizo kufa kwa kudanganywa na Mganga wa kienyeji?
Hebu fikiria mtu mwenye akili timsamu katika kizazi hiki yaani mwaka 2023, anambiwa angefika mbinguni haraka ikiwa wangekufa kwa njaa na Mchungaji wao Paul Mackenzie, sasa utasemaje ni uwongo habari za 1805?
 
Kama pamoja na maaendeleo ya sasa, utandawazi, elimu na mitandao, bado watu wanakufa wakikanyaga mafuta ya mwamposa.

Sembuse watu enzi hizo kufa kwa kudanganywa na Mganga wa kienyeji?
Anaona ishu kumwamini mganga

Wakati watu siku hizi wanaamini ukiweka buku mchezo supa unapiga milioni 🤣🤣
 
Back
Top Bottom