Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Mosi,Kukaa kimya kuna nguvu zaidi kuliko pale unapotaka kudhibitisha ukweli au kujitetea. Na hii kweli kabisa wakati mwengine unaweza kupata kashfa ambayo jinsi kadri unavyotaka kujitetea unajikuta unazidi kuharibu,kwahiyo wakati mwingine kunyamaza ni jibu zuri sana,watu wanabaki njia panda
Pili, Pale uaminifu unapokosekana basi hata kuomba samahani hakuna maana yoyote ile,ni kweli kabisa ukishapoteza uaminifu mara nyingi sana kuomba msamaha hakuna uzito wowote ule,kwahiyo hakikisha unaaminika siku zote
Tatu, Siku zote vitawale vitendo vyako au mihemko yako na ujifunze kutochukua hatua haraka,mara nyingi sana tunapopata maudhi au kukerwa haraka sana hupandwa na kisukari na kufanya maamuzi ya haraka bila tafakuri matokeo yake tuna juta baadae,chukua hii mara ukipata ghadhabu vuta pumzi ndefu mara tatu itakusaidia.
Nne,Unapokuwa muaminifu utawapoteza watu ambao hawastahili,iko hivyo siku zote ebu hapo kazini kwako mnapopiga madili,jifanye wewe ni muaminifu utaona utakavyotengwa na wapigaji
Tano, Moyo mmoja mzuri na wenye ukarimu ni bora kuliko sura nzuri 1000
Sita,Kuwa na marafiki wachache,maisha yako binafsi,akili huru na kuwa na moyo mzuri
Saba, Kamwe usiende tena kwa mtu ambaye alikuacha
Nane, Acha kuwaza sana kupita kiasi kwani hauwezi kudili na kila kitu maishani
Tisa, kama kuna mpumbavu mmoja anaondoka katika maisha yako basi kuwa muelevu sana kumuacha aende zake
Kumi, marafiki wa kweli ni wachache sana kuwapata,basi ukiwa nao hakika wewe una bahati sana
Nawapenda sana
Ni hayo tu!