Kuna jamaa yangu,alikuwa ana date na mtoto wa mchungaji jamaa hajui hili wala lile,jamaa akaitwa church na huyo demu! Alipoenda dem akamkuta yupo peke yake, ana kikombe cha maji na sindano,wamekaa weee kisha demu akamuingizia mada ya agano la damu! Jamaa akakubali, demu akamchoma na sindano mkononi kisha binti nae akajidunga wakachanganya damu wakanywa, aise aliponisimulia nilishangaa na kuona kuwa jamaa na huyo binti basi mpaka kifo. Ila kwa sasa jamaa anasema ilikuwa ni upuuzi tu manake wana miaka mitatu sasa hawana mawasiliano na kila mtu ana maisha yake.