Kuna ukweli wowote mwanamke akiwa ameshika ujauzito ataanza kupata na muwasho katika sehemu zake za siri

mtoto wa kipare

Senior Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
187
Reaction score
196
Habari za jumapili wakuu.
Naombeni kujua ili kuondoa Utata, Eti pana ukweli wowote kwamba mwanamke akiwa ameshika ujauzito kwamba ataanza kupata Na muwasho katika sehemu zake za Siri, Nikiwa Na maana kutokwa Na uchafu mweupe ambao upo kama mtindi?????
Je, pana ukweli wowote hapo.

Nawasilisha!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli inaitwa vaginal Leukorrhea anatoa uchafu unakua mwembamba na kama maziwa hivi
Ila nakushauri umpeleke kituo jirani cha afya au akienda clinic awaambie hilo tatizo maana kuna fungus pia anasababisha kutokwa na uchafu mweupe


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hakuna ukweli. Kama unapata hivyo vitu, wahi matibabu
 
Nimewahi pitia hiyo stage, sikuwahi kupata muwasho wala hivyo vingine. Basi tuseme si wote hupata changamoto hiyo
 
huo unaokuwa kama mtindi na muwasho juu sio kawaida mkuu, ni fangasi wazi kabisa, watu wanasema ni kawaida maana ukweli ni kwamba huwa inawakumba wajawazito wengi ni sababu ni kuwa mwanamke anapokuwa mjamzito kinga ya mwili huwa inashuka kidogo ili kuruhusu kiumbe/kitu kipya (mtoto) kisikataliwe (rejected) na kinga ya mwili.

Mwambie ajitahidi tu usafi na kula balanced diet

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…