Kuna ulazima gani wa vyeti na mashahidi?

Kuna ulazima gani wa vyeti na mashahidi?

M.E.M.A

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
1,373
Reaction score
472
Nimekaa na kufikiria ya kwamba:

Mara nyingi tunawaambia wenzi wetu tunawapenda, na pia wakati wa kufunga ndoa tunatoa viapo na mwisho wa siku tunakabidhiwa 'a piece of paper' kuashiria muunganiko wa wawili wa wapendanao.

Sasa basi mama wanapojifungua hamna viapo wanavyokula vya kuwapenda, kuwatunza na bla bla zinginezo na pia hakuna cheti wanapewa kwa ajili ya muunganiko huo. Ila utakuwa na kukuwa na kujisikia unajaliwa na unapendwa. Je kwanini tuamini kuwa kile cheti ndio uthibitisho pekee wa muunganiko wa watu wawili? Na je ni wakati gani najisikia nimeoa au nimeolewa..? Na ina maana kinachowafungamanisha wawili ni kiapo na kile cheti? Na kama cheti ni muhimu, je kikipotea au nikikichana au kukichoma moto ina maana ndoa ndio imeisha? Mmh

(Kama nimepotea forum nisameheni, ila naamini hapa ndio pake)
 
Back
Top Bottom