Kuna ulimwengu usioonekana?

Kuna ulimwengu usioonekana?

Niliota kuna jamaa kaniwekea sumu kwenye beer ya seringeti, kesho yake sikwenda kijiweni, nilipofanya utafiti wa kina nikagundua kulikuwa na huo mapango. Sasa nimehama kijiwe, ndoto ni ulimwengu wa roho, unaweza kutonywa na mababu zako.
Hiyo ilikuwa ndoto maono
 
Kuna mtu mmoja ambae nina uwezo wa kutamka kitu leo kumuhusu kesho tukiona anakuja kunithibitishia nilioyasema jana bila kufahamu kinaendelea nini kwake.

Hii imekaaje mkuu?
 
Niliwahi kuota marehem mama ananikataza kutumia mafuta ya nabii fulani,mpaka leo siyatumii kabisa
 
Si wa kiroho bali uko katikati ya kiroho na kimwili na pengine huo ndio unapokea cords toka kwenye ulimwengu wa roho na kuzibadili na kuzitafsiri kwenye ulimwengu wa kimwili.

Niliwahi kuripoti kituo cha polisi wiki nzima lakini hiki kituo hakikuwa halisi... Yaani kila fahamu zikinijia nilijikuta tayari nimetoka kuripoti ila sikujua kwa mashtaka gani.

Nitaendelea

Nilimuomba Mungu akanipa uwezo huu wa kuona ktk Ulimwengu wa Roho na Sasa ninaona...

Ni Raha sana ila inabidi uombe hekima
DOMSHA School of Spiritual Awakening
Nataka nianze chekechea
 
Unapokuwa umelala roho huacha mwili na kwenda kuzurura huko kwenye huo ulimwengu. Sio wote huwatokea hii hali ila kuna ndoto unaota unajua kabisa umefanya jambo flani na ulikuwa na ufaham wako ila kukicha unagundua ni ndoto.
Mfano mm huwa naota napaa angani na huwa nipo nusu nimelala na nusu nipo macho. Ila nikiamka nagundua nlikua naota na unajihisi kabisa 7naweza kupaa
 
Ulimwengu wa Roho ni mpana...

Na kila mtu ana kiwango chake cha kuona kulingana na Mungu alivyomjalia...

Wengine ni waota ndoto, wengine wanamaono...

Huko kuna watu kama wewe, kuna wachawi, wanyama, mizimu, wapo

Nikianza na vita, kila mtu anavita vyake ambavyo anapigana navyo uwe unaona huoni ila unavyo...

Kuna neno linasema kupigana kwetu sio kwa damu na nyama bali ni kwa Roho...

Huko kwenye Ulimwengu wa Roho, kuna vita ya wewe na wakuu wa giza, hapa na wewe unaona majeshi ni kama watu wakati mwingine uweza ona wanyama ila unapigana nao kama una nguvu za Rohoni unawapiga na unashinda kama huna nguvu unashindwa...

Kuna kushinda na ukishinda kule na huku Ulimwengu wa mwili umeshinda...

Kuna mambo yajayo...

Hapa kama kuna jambo linataka kutokea Liwe zuri au baya kwako, familia, jirani, nchi unaona...

Kwasasa mimi ninaona mpaka yatayotekea nchini...

Kusema nogopa...
Naweza kusomea hayo mambo?
 
Tunaishi ulimwengu huu. Baada ya hapa ipo Astral World. Halafu ipo Brahma World. Hapa ndipo wanapokwenda watu baada ya kufa hapa duniani. Baada ya hapo ipo Patra World, ambapo ndio wapo watu waliopiga hatua zaidi, kama vile Aristotle, Socrates, Leonardo da Vinci, Winston Churchill, na wengineo. Halafu bado, inaendelea. Zipo dimensions nyingine.
Tupe somo mkuu

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Si wa kiroho bali uko katikati ya kiroho na kimwili na pengine huo ndio unapokea cords toka kwenye ulimwengu wa roho na kuzibadili na kuzitafsiri kwenye ulimwengu wa kimwili.

Niliwahi kuripoti kituo cha polisi wiki nzima lakini hiki kituo hakikuwa halisi... Yaani kila fahamu zikinijia nilijikuta tayari nimetoka kuripoti ila sikujua kwa mashtaka gani.

Nitaendelea
Aisee!
 
1736506355718.jpg
 
Tunaishi ulimwengu huu. Baada ya hapa ipo Astral World. Halafu ipo Brahma World. Hapa ndipo wanapokwenda watu baada ya kufa hapa duniani. Baada ya hapo ipo Patra World, ambapo ndio wapo watu waliopiga hatua zaidi, kama vile Aristotle, Socrates, Leonardo da Vinci, Winston Churchill, na wengineo. Halafu bado, inaendelea. Zipo dimensions nyingine.
Ningependa haya yote uliyoyaeleza, niyapate kwa ufafanuzu mzuri, maana ni elimu kubwa sana hii!
 
Back
Top Bottom