Kuna umuhimu gani wa kuwekeza katika mpira bongo?

Kuna umuhimu gani wa kuwekeza katika mpira bongo?

crankshaft

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,427
Reaction score
3,438
Singida united ilikuwa timu kubwa na uwezo wa kusajili wachezaji wakubwa bwana yule alipokuwa madarakani. Ila alipotumbuliwa tu timu ikaparanganyika mpaka kupotea kabisa kwenye ramani ya soka bongo.

Baada ya kurudishwa tena madarakani wameibuka tena na timu singida big stars na inafanya matumizi makubwa pesa haijulikani zinatoka wapi. Tafsiri yake akitumbuliwa tena huyu mwamba timu inarudi tena jalalani kwa sababu wanachama wake hawawezi kuiendesha kama ile ya kwanza.

Kama timu kama yanga ilikuwa inatembeza bakuli maana yake siku gsm au mo wakiamka vibaya na kuamua kujitoa kudhamini mpira tutarudi matopeni.

Jana majimaji wameshindwa kulipia gharama za hoteli dar na kulazimika kubaki huko kwa wiki mbili huku wakitembeza bakuli wapate nauli na gharama za hoteli ya watu.

Mmiliki wa gwambina katupa timu kama takataka na kuwaambia wachezaji wasambaratike wakatafute timu na timu kaifuta.

Katika mazingira kama haya kuna umuhimu gani wa kuwekeza katika soka bongo?
 
Kumbuka bakuli la Utopolo ndo utajua umuhimu wa timu kuwa na Mwekezaji.
 
Inawezekana kabisa Yanga inaendeshwa kwa ruzuku. Hao GSM ni geresha tu.

Huko duniani matajiri ndiyo wananunua timu. Hapa kwetu watu wanajaribu kumiliki timu ili kuutafuta utajiri na kutumia kama kichaka cha ufisadi na uhujumu uchumi.
 
Back
Top Bottom