Kuna umuhimu kuwepo Taasisi ya kusimamia NHIF

Kuna umuhimu kuwepo Taasisi ya kusimamia NHIF

DidYouKnow

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
1,229
Reaction score
1,950
NHIF kwa sehemu kubwa imekuwa ni imehodhi utoaji wa Huduma za Bima za Afya kwa Tanzania. Kwa bahati mbaya sana, serikali kwa mkono mwenyewe imekuwa ikiipa kiburi NHIF kwa kufanya kila namna kuua kampuni za bima za afya binafsi. NHIF imepewa ukuu mkubwa hadi wa kutengeneza package (wanaita Price Schedule) ambazo mtoa huduma anapaswa kuzifuata.

Bahati mbaya, utengenezaji wa hizi price schedule si shirikishi, na hata gharama zake nyingi zina ukakasi. Ukitoa huduma kwa mwanachma wa NHIF, wao wana nguvu ya kuamua watakulipa kipi kati ya huduma ulizotoa, watakukata kiasi gani, bila kuwapo na sehemu ya kukata rufaa. Wao watakaloamua ni FINAL.

Kama kawaida ya NHIF, huwa wana tabia ya kutoa document ya price schedule kama unofficial document na kisha kusikilizia wadau wanasemaje. Wanafanya makusudi ili kusoma upepo, hii ni dalili kwamba hawa viongozi huwa hawana nia njema.

Kuanzia jana, viongozi wa NHIF wametoa price schedule wanayosema itaanza effective Julai Mosi 2021 kujaribu kuona wadau watapiga kelele gani. Document hii inasambaa miongoni mwa wamiliki wa vituo vya afya na madaktari. Ina mapungufu mengi sana kama kawaida yao, lakini jambo la muhimu sana, Serikali inapaswa iunde chombo cha usululishi wa migogoro itokeayo kati ya NHIF na Wadau - wanachama na wamiliki wa vituo vya afya.

Kwa haraka haraka naweza orodhesha mapungufu haya

1. Kusisitiza kwamba huduma zitolewe kulingana na National Essential Medicines List (NEMLIT) - NHIF hukata huduma ambazo zimetolewa nje ya NEMLIT, wakati huohuo, kuna dawa na vipimo ambavyo vimeorodheshwa kwenye NEMLIT wao hawavitambui.
Screenshot_20210624-191607_Google PDF Viewer.jpg

2. Malipo ya Consultation - Hapa Tanzania consultations fees kwa daktari hulipwa ndogo sana. Kabla ya hii document ambayo watakuja kuiita fake kuja, Consultation ya Daktari asiye specialist hospitali ilikuwa inalipwa 10,000/=, Specialist 25,000/= na Superspecialist 35,000/=. Sijajua NHIF wametumia kigezo gani kushusha hizo consultations kuwa 7,000/=, 15,000/= na 25,000/= kwa mfuatano. Wana base yoyote waliyotumia?
Screenshot_20210624-191227_Google PDF Viewer.jpg

3. Malipo ya huduma za Malazi (Inpatient)
Nimeshangaa kuona malipo ya Huduma ya Malazi yako tofauti kati ya National Referral Hospitals na Zonal Referral Hospitals wakati level ya utaalamu ni ileile. Wataalamu walioko kwenye National Hospitals na Referral Hospitals wana level sawa. Sasa kitu gani kinawafanya wagonjwa wanaolazwa kwenye Zonal Referral Hospital walipiwe 35,000/= kwa siku na wale wa National Hospitals walipiwe 40,000/=? Linalolipwa ni jina la hospitali? Au kwa sababu hizi zonal hospitals ni hospitali za mashirika ya dini?
Screenshot_20210624-191315_Google PDF Viewer.jpg

4. Kwa makusudi kabisa, NHIF imekataa kuzitambua ICU za hospitali nyingine zote nchini Tanzania isipokuwa ya Muhimbili National Hospital. Hivi ICU ya MNH ina nini? Wagonjwa wanaolazwa kwenye ICU nyingine wanawatambua kama HDU. Huu ni uhuni wa wazi. ICU ya MNH mgonjwa analipiwa 500,000 per day wakati ICU za hospitali nyingine hata Benjamin Mkapa wanalipiwa 60,000/= wao wakidai ni HDU.

5. Kuzuia baadhi ya dawa kutolewa katika ngazi ya Hospitali za Rufaa za Mikoa kushuka chini.

Ni kweli kwamba hapo nyuma hospitali za mikoa zilikuwa hazina madaktari bingwa. Lakini sasa hospitali hizi zimesheheni madaktari bingwa. Lakini wanazuiwa kutoa dawa ambazo daktari bingwa wenzao walioko hospitali za kanda na taifa wanaruhusiwa kutoa. Wanaogopa nini kuwaruhusu kutoa dawa hizi?

6. Kuzuia mgonjwa aliyeonwa hospitali ya Taifa au Kanda kwenda kuonwa kwenye kliniki ya madaktari bingwa ndani ya mwezi husika. Najua mantiki ya hii ni kuzuia madaktari bingwa wasihamishe wagonjwa toka Hospitali za Serikali. Lakini hii si kazi ya NHIF. NHIF wafurahie kuona mwanachama wake anapata matibabu sahihi. Wasimchagulie mwanachama sehemu ya kwenda kuchagua matibabu.
Screenshot_20210624-201423_Google PDF Viewer.jpg

7. Kuzuia wanafunzi waliokata bima ya afya kutumia huduma za ujauzito, na baada ya kujifungua si sahihi. Hasa katika kipindi hiki inaposisitizwa mtoto wa kike apelekewe shule.

8. Kufanya vipimo vya msingi kama ECHO viombwe kufanywa na daktari bingwa tu.

Hii imenishangaza sana. Sijui kuna madaktari waliosomea nini huko NHIF. Nadhani kuna umuhimu wa baadhi ya watumishi wawe wanahamishwa maeneo yao ya kazi wakajifunze sehemu nyingine. Yaani Echocardiography iombwe na specialist? Mbona hata clinical officer anajua kwamba mgonjwa huyu anahitaji kufanya ECHO? WHAT DO YOU WANT TO SAVE?

9. Kwanini kuwe na gharama tofauti za kipimo kama Echo? Kuna sehemu ni 40,000/=, sehemu nyingine ni 55,000/= na sehemu nyingine ni 100,000/=. Huo ni uhuni tu. Kama mnataka echo ziwe na bei tofauti basi wekeni bei kulingana na level ya anayefanya. Kama kuna superspecialist hospitali ya Mkoa au JKCI wakifanya Echo itakuwa ni ileile tu tusidanganyane.

10. Nimeangalia gharama zenu za vipimo hadi nimecheka. Hivi kweli mnafanya cost analysis? Nasikia hamna wataalam wa Maabara. Mnacheza tu na Excel. Kuna tests unashangaa bei zake. Mfano Sputum Culture and Sensitivity mnasema 15,000/=. Hivi mnajua vitu gani vinatumika kufanya isolation ya organism halafu baadaye mtu afanye drug susceptibility test? Nyie ndio mnachangia kwa kiasi kikubwa kutengeneza drug resistance, maana hospitali zinashindwa kufanya tests hizi kwani ni hasara. Ajabu sana mtu akikataa kutoa huduma hizo mnamfungia.

Kwa ufupi NHIF mnahitaji mtu wa kuwa control. Mmejiachia sana.

Screenshot_20210624-191527_Google PDF Viewer.jpg
 
Kujiunga na kukatwa pesa kwenye mshahara wa mtumishi wa umma kwa ajili ya NHIF ni suala la lazima (mtumishi hana uchaguzi wala uamuzi), lakini linapokuja suala la kupewa huduma, linageuka kuwa suala la vigezo na masharti mazito.
 
Anamsimamia NHIF kweli?.ana hio mandate?
Sio kuwa anasimamia Kampuni Binafsi za Bima?.
TIRA ni Regulator tu.

NIHF iliyumba baada ya serikali ya Magufuli kujiondoa kwenye suala la kuchangia mfuko kama alivyofanya kwa NFRA.

Kiukweli binafsi mpaka leo nimeshindwa kujua yule mzee pesa alikuwa anapeleka wapi.

Kilichotokea gharama za huduma zikawa ni kubwa kuliko michango ya wanachama wa NHIF.

Sasa katika kuunusuru mfuko kutokana na madeni ndio bodi ya NHIF ikiongozwa na Makinda wakaamua kuunda vifurushi vipya kama unavyoviona ili usife. Na kila mwenye akili timamu alilalamika.

Magonjwa mengi yameondolewa na gharama za uchangiaji zimepanda.
 
TIRA ni Regulator tu.

NIHF iliyumba baada ya serikali ya Magufuli kujiondoa kwenye suala la kuchangia mfuko kama alivyofanya kwa NFRA.

Kiukweli binafsi mpaka leo nimeshindwa kujua yule mzee pesa alikuwa anapeleka wapi.

Kilichotokea gharama za huduma zikawa ni kubwa kuliko michango ya wanachama wa NHIF.

Sasa katika kuunusuru mfuko kutokana na madeni ndio bodi ya NHIF ikiongozwa na Makinda wakaamua kuunda vifurushi vipya kama unavyoviona ili usife. Na kila mwenye akili timamu alilalamika.

Magonjwa mengi yameondolewa na gharama za uchangiaji zimepanda.
Hehe pesa ilienda Miradi ya Maendeleo, ndege nk
 
Back
Top Bottom