The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mara kadhaa linapotokea tukio la utekaji bila ya uwepo wa ushahidi wa Video Polisi wamekuwa wakisema wahusika ni watu wasiojulikana mfano Tukio la mzee Kibao, Abdul Nondo na wengine wahusika hawajajulikana mpaka sasa.
Matukio kama hayo yakitokea na muda mfupi video za CCTV zikiachiwa utasikia polisi wanatoa taarifa kwamba walienda kukamata wakati huo hawana uniform wala gari ya jeshi la polisi mfano mzuri ni tukio la kukamatwa kwa mwenyekiti wa CHADEMA Iringa mjini Frank Nyalusi.
Pia hili la Polisi kudaiwadaiwa kuvamia Ofisi za "Reachout Tanzania", wakidai kumtafuta Wakili Lusako Alphonce, ambaye hakuwa ofisini.
Maoni yangu tukio likitokea tusubiri taarifa ya polisi alafu video ziwekwe hadharani ili wajikanyage vizuri.