Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Taasisi hii ilianzishwa kwa lengo la kupambana na rushwa, na pia taasisi hii haikuanzishwa kwa lengo la kukamata wala Rushwa wadogo Pekee bali walaji wa aina zote wa rushwa.
Mara nyingi sana tumekuwa tukisikia viongozi wakiwaamrisha maafisa wa Takukuru "kamata yule weka ndani" lakini wengi wa wanaokamata ni watendaji wadogo wa Serikali kama vile Watendaji kata, polisi, walimu, Nk lakini ni ngumu viongozi wa juu wa Serikali Takukuru kushughulika nao ama kuwakamata.
Ripoti ya mkaguzi mkuu wa Serikali ilibainisha kila Aina ya ubadhirifu wa pesa tena katika idara nyeti ,lakini hatukuona. Wala kusikia Takukuru kumshikilia yoyote kwa uchunguzi.
Leo chombo kikubwa kama Takukuru kinafanya kazi kwa maagizo tofauti na hapo ni kimya.
Je, umuhimu wa Taasisi hii upo wap?