Kuna umuhimu?

B_E
Ningejikaza kisabuni..halafu ningemjibu.." uliona wengi baba, lakini hapa kwangu ndo breki yako..mwisho wa njia! "
Ila uongo si kazi..ningeumia sana rohoni na ningemchukia sana!


mie kuweka kitu rohoni jamani kitanitesa sana, uwiiii! ningehoji mpaka kieleweke, yaani cnaga ule uvumilivu wa kusema wacha nife nalo rohoni labda iwe imeshindikana but zile za hapo kwa hapo kukuhoji ni muhimu, may b kuwe na wageni/2po sehemu ambayo ctaweza kuhoji kwa wakati huo but nikipata muda tu ndio jambo la kwanza aisee.
 



majibu mengine yanakatisha tamaa jamani, khaa! ukipata wa nje hapo na akijua ndoa huna mrs.
 
jamani... hii mada!
Labda niulize swali kwa akina baba/kaka
Hivi kwanini mnapenda kujua ya zamani? Ukishajua ili ufanyeje? wanawake wengi hawatakuambia ng'oo maana wanajua hiyo info utakuja kuitumia baadae against them.Ni kama mlinzi wa amani anapochukua maelezo yako ya ziada - tofauti ni kuwa nakutahadharisha kuwa hayo maelezo baadae yanaweza kutumika kama ushahidi mahakamani!
"MAHAKAMA za wenye ndoa" - huwa ni chumbani..usiombe!! - ni mtuhumiwa na hakimu/jaji hakuna cha shahidi wala nini! Je haki hapo itatendeka? Mshtakiwa/mtuhumiwa akiona kesi inamwelemea anaruka dhamana potelea pote maana hata hiyo dhamana anajipa mwenye maana haipo!
 

Historia siku zote ni muhimu kwani historia huwa ina tabia ya kujirudia. Be careful. Kudharau historia, ni kwenda bila kujua utokako!

Binadamu siku zote huwa ni mujumuisho wa linalotokea leo, kesho, .... mpaka utakapokufa. Kila linalotokea huacha alama yake katika maisha yako na usipoangalia hayo, the chance of failure ni kubwa mno.

Tatizo ni je unauliza historia hiyo lini. Kuna mtu ameshasema hapa historia ni muhimu kabla ya commitment. Tena iwe yoote nzima nzima. Halafu ifuate comitment. Ukifanya comitment bila kujua historia, unaogelea kwenye bwawa ambalo hujui kina chake. Siku zote kuna hatari.

Tabia za watu zinajengwa na yaliyokwisha wakuta. Tujiheshimu leo, vinginevyo historia itatuhukumu. Mwanamke aliyekuwa anafanya kazi Ohio, kazi ya kujiuza, ana mtazamo fulani kuhusu mahusiano. Mtazamo ndio unaomfanya mtu awe vile alivyo. Ni muhimu kuelewa mtazamo wa mtu KABLA NA NIRUDIE TENA KABLA. Huwezi kujua mtazamo bila kujua alifanya nini huko nyuma.

Ukiwa loose leo, uwezekano wa kuwa loose mwaka ujao ni mkubwa. Hivyo kujua ni muhimu, tena ujue yoote. If you have no balls to stand them, you will have no balls to stand the relationship.
 

I get you loud and clear Mkuu!
Tatizo linaanzia na wewe mwenyewe na mahali ulikompata huyo unayetaka kufunga naye pingu.Na ndiyo maana mtu anashauriwa achunge sana anakopatia mke/mume wake wa baadae maana inaweza kuja kumgharimu baadae.Kama mmekutana sehemu zenye utata, jipe muda wa kutosha kumfahamu.Usikutane na binti leo, baada ya miezi miwili ukatangaza ndoa!Kama mna uchumba wa muda wa kutosha, huhitaji kumpa interview kujua historia yake, bali through observation na mambo mengine, historia yake itajichora bila wewe kuingia gharama au kutumia nguvu nyingi.
Ukiwa na mtu kwenye uhusiano, utaona vijitabia ambavyo vinaashiria kuwa huyo si wa kuoa au kuolewa.
 


Nadhani mchumba kama akitaka kujua historia yako ni vema na haki yake. Unao wajibu wa kumwambia ukweli ili afanye maamuzi huku akijua ukweli wote. Kuogopa kuweka wazi historia yako (hasa kwa Mchumba wako) ni kutojiamini na kimsingi inaweza kubatilisha ndoa.

Kuna ndoa ya kikristo ilibatilishwa kwa sababu kama hizi: Mwanamke katika ujana wake alitoa mimba lukuki na katika incidence ya mwisho ya kujaribu kutoa mimba alipata matatizo na kuharibu kizazi na kupoteza uwezo wa kushika mimba tena (at least from medical point of view!). Hata hivyo dada huyu hakuliweka hili wazi kwa mchumba (si mmojawapo ya waliohusika na mimba zilizotolewa!) wake kwa kuhofia kumpoteza. Hata hivyo ukweli ulikuja kujulikana kwa sababu kwanza hakuweza kushika mimba na walipokwenda hospitali ukweli ulikuwa wazi. Kanisa lilisema ndoa haikuwepo in the first place kwa sababu mwanamke pamoja na kujua hiyo fact aliificha!

Ndoa ni mkataba na hivyo ni muhimu kila upande kudisclose all the facts ambazo kama upande wa pili ukijua unaweza kukataa kusaini/kuingia kwenye huo mkataba.

Kama historia yako kwa sehemu kubwa ipo tayari kwenye public domain (hata kama kwa wakati huo muhusika haijui) ni vema akaisikia kutoka kwako. usipomwambia, kwa namna moja ama nyingine anaweza kujua halafu itakuwa mbaya zaidi.

Akipata taarifa zako (pengine chafu!) kutoka kwa watu wengine itapunguza uaminifu wake kwako na pia watu wengine wanaweza kuongeza chumvi kwenye hiyo historia na kufanya uonekane mchafu zaidi. Maadui wa ndoa/uchumba wanaweza kutumia mwanya huo kuharibu ndoa/uchumba wenu. Lakini kama tayari ukweli uliuweka wazi hata akisikia kutoka huko nje atapuuzia tu na kuona watu hao ni wachonganishi.

Ni kweli ukweli huo unaweza kuumiza, lakini kwa mtu mwenye busara hilo ni bora kuliko kuja kujua ukweli huo kupitia watu wengine. Kwa mtu anayejiamini, anayejua kupenda kwa hakika hana sababu ya kumficha mwenza wake kitu chochote.

Kama manapendana ni vema mambo yote yakawa wazi. Binafsi nasisitiza uwazi huo juu ya historia yako ufanyike kabla ya ndoa na si baadae.

Ukweli mara zote utakuweka huru!
 
Je!kuna umuhimu wowote kwa wachumba,au wapenzi kuelezana historia zao za kimapenzi za kipindi cha nyuma kabla hawajakutana?...

...swali la nyongeza;

Idadi ipi ya wapenzi waliopita ni muafaka kumtajia mwenzako hata kama unadanganya?

1. kwa wanaume

2. kwa wanawake

...kwa experience yangu, wanawake wengi husema, "...wanaume watatu tu", wengine...."... hawafiki watano!"
 

Mbu,
Naweza nikasema kuwa wanawake haiwasumbui sana kutaka kujua kabla yangu walikuwepo akina nani.Kinachoweza matter ni je, sasa katulia? kwa wanaume ni tofauti..wengi utasikia wanalilia waoe wanawake ambao hawajaguswa na mtu ilhali wao kila kukicha wanakimbizana na sketi!
Nataka nimnukuu Oscar Wilde - huyu ni mwandishi na mtunga mashairi wa huko Uingereza aliyebobea kwenye mambo ya uhusiano japo yeye mahusiano yake yalikuwa na utata sana by standards za kipindi kile alichoishi cha karne ya 19.
"Men always want to be a woman's first love. Women have a more subtle instinct: What they like is to be a man's last romance"
 
jamani... hii mada!
Labda niulize swali kwa akina baba/kaka
Hivi kwanini mnapenda kujua ya zamani? Ukishajua ili ufanyeje? wanawake wengi hawatakuambia ng'oo maana wanajua hiyo info utakuja kuitumia baadae against them...

...duh!... kama huko awali alishaziporomosha kwa fujo kiasi kwamba sasa kila akidaka zinabanduka? am sure ushawahi sikia 'kizazi kilicholegea'...
 
...duh!... kama huko awali alishaziporomosha kwa fujo kiasi kwamba sasa kila akidaka zinabanduka? am sure ushawahi sikia 'kizazi kilicholegea'...

Mkuu,
Nadhani japo tumejadili sana hii ishu, kuna kitu tumeki overlook.
Ni mambo gani ya ku declare.Nadhani kuna mambo ya kimsingi sana mtu anapaswa kuyasema kwa mwenzie hasa kama kuna dalili ya kuwa na uhusiano wa muda mrefu.Kwa uchache nitayataja na nitaomba wengine waongezee kwenye listi:
1. Alishazaa - ( wote mwanamke na mwanaume)
2. Kuwa na hali ya kutoweza kuzaa ( wote)
3. Magonjwa hatarishi kama UKIMWI ( wote)
4.Kuwa na ndoa nyingine ( wote)
sijui kama ni kitu cha maana kutaja ulishalala na watu wangapi kabla ila kama ni lazima ( wote)
5.Kuwa na perversive tendencies ( tigo, chumvini,kupiga chabo etc) -( wote)
6.Ulishatoa mimba au kusaidia kutoa mimba ( wote)


ongezeeni kwenye listi
 

...Now you are talking πŸ˜€...

ndio maana nasema kuna umuhimu sana kujua. Akili kumkichwe tu yepi ya kusema na yepi ya kuyahifadhi.

Kwa mfano, sio busara kumwambia mkeo/mumeo... "fulani pekee ndiye aliyekuwa ananifikisha kileleni kuliko hata wewe na wenzako wote nilowahi kukutana nao kimwili!"
 

Hii kali!
 
.. Nyie msijidanganye mwayego hakuna kitu kisichoeleweka kwa wanaume kama kumwambia idadi (na pengine majina ya waliopita kwako) utakoma utakuwa unasimangwa kila siku hata siku ukichelewa kidogo utasikia au ulikuwa na flani yaani afanya kujichagulia tu leo amtaje nani kesho nani acheni kabisa . Wengine tunatamani kurudisha siku nyuma ili tu upate nafasi ya kurekebisha maelezo maana ningejua ningesema sijawahi na kustick hapo na angeniuliza ilitolewa na nani ningesema nilikuwa mchazaji mzuri wa rede na shekirede sijui rede sheki........
 

Yaani u made my day, nimecheka mpaka.....Yaani uliyosema ni kweli tupu....Hili ni somo kwa watu wapya, kama una mtoto labda ndio useme vinginevyo...achana na biashara ya kuandika historia mpya kwa ku'kasuku' ya kale....
 
Yaani u made my day, nimecheka mpaka.....Yaani uliyosema ni kweli tupu....Hili ni somo kwa watu wapya, kama una mtoto labda ndio useme vinginevyo...achana na biashara ya kuandika historia mpya kwa ku'kasuku' ya kale....

.. Da mkubwa we acha tu😱.
 
Hajatulia wala nini, nimefata ushauri wake, kwa hiyo najivijali kama kawa.

Mrs. Mtaba mumeo naona ana hasara ya kufa mtu. Tulia please si unajua tena bucha zote zinauza the same type of meat. Otherwise split legally and u'll be fine.

Ni mtazamo tu
 
List ya mambo ya kumwambia mtu ambaye unatarajia awe mwenzio haitakiwi iwe na kikomo. Kila kitu ambacho unaamini akikijua, au akigundua baadaye itakuwa soo lazima ukiseme.

OK kuna wanaosema ukimwmbia baadaye itakuwa ndo subject ya kukusimangia. Kwa mfano umemwambia ulishakuwa na uhusiano na fulani, siku akikukuta naye atakuwa issue ndefu. OK, hii ni kweli.

Imagine mtu anayekusimangia kitu ulichomwambia mwenyewe, aje kujua kitu hicho bila wewe kumwambia. It will be worse. Unaweza kujisafisha kuwa si kweli, but anaweza akapata sure evidence. Kwa mfano umemficha kuwa ulikuwa na uhusiano na mtu. Na huyo mtu ameshakuona naye mara kadhaa ila unamwambia hakukuwahi kuwa na kitu. Siku ya siku anakutana labda na picha mlizopiga wakati ule. Na ameshakuona naye mara kadhaa na hukuwahi kudisclose. Hiyo inaweza isiwe masimango tuu, it may break you completely.

Halafu, kitu chochote ambacho haujisikii vizuri kumwambia mwenzi wako, ujue ni kibaya. Kwa sababu relationship mnayoenda kuingia ni more serious kuliko hicho kitu. Ujue siku zote kitakuwa na matatizo kwako. Siri humuumiza zaidi yule anayeitunza. Kuna healing inatokea unapoisema siri. You keep it at your own detrement. Siku zote utajiona hauko sawa kwa sababu kumbukumbu mbaya ambazo hazijatolewa nje will haunt you always.

Sema, akukatae au akukubali hivyo ulivyo. Atakuheshimu na wewe utajiponya. Mdanganye ujiumize mwenyewe.

Kitu cha kusema ni kile chote ambacho kinakusumbua na unahisi akikijua anaweza kuchukia au kufanya maamuzi mengine kama ya kukuacha. Kiseme kwa sababu hicho ni sehemu ya personality yako.

Usilazimishe uhusiano. Hayo ndo huleta balaa na kufanya mahusiano mengi hasa ndoa ziwe ni mzigo kwa wanandoa badala ya kuwa relief. Mbwagie yote ayakatae au ayakubali. Hata akikusema baadaye, wakati wewe ndo ulimwambia, bado unanguvu ya kumtaka asikuumize kwa mambo uliyokwisha mweleza.

Siri hazifai na siri huvunja hasa ndoa. Wengi baada ya kujua siri walizofichwa ndo maana huanza ku-react na kufanya mambo ambayo ni damaging to themselves and their lovers.
 
kwa experience niliyo nayo, kuna wakati mnajikuta mmetulia sehemu, ww na mwanamke wako (mara nyingi huwa ni chumbani). pale stori huanzia kusikojulikana na mwanamke huanza kuongea yale aliyopitia awali, yaani maisha ya kimapenzi. ila kuna mambo mengine atayaficha ila ukiwa mjanja waweza kuyajua. ukianzisha ww kutaka kujua undani wake hutafanikiwa. mwache mwanamke atumie hisia zake kukueleza (kama utapenda) kwa wanaume...sidhani kama ni wawazi kiivyo
 

Ndiyo wanawake si wawazi kihivyo. Hata wanaume si wawazi kihivyo. Na hiyo ndiyo sababu ya milolongo ya matatizo tunayoyaona; mara nyumba ndogo, sijui nini... Sababu zake ni kukosekana kwa uwazi. You come to realize when it too late and you say to hell. Ukiona mwanaume anahamia nyumba ndogo na kutelekeza familia, si bure. Huwa kuna reasons na kwa kuwa wanaume hawalalamiki publicly, huwezi jua. Mara nyingi wanawake wana-play victim even when they are the source.

Siri ni kumbana mapema na kumtaka awe wazi. Kuna mtu ukijua mke wako alishawahi kutembea na fulani even if walifanya mapenzi ya kawaida, ile kujua tu can make you mad. Ndio wanaume tulivyo. Sasa fikiria umejua through a third party na ukajiridhisha kuwa kakudanganya yaani alikuwa na uhusiano na fulani hafu hujui!!! It tells alot. Sababu ya kuficha ni kuwa kuna uwezekano wanaendelea na uhusiano huo. Kwani mambo hayo tunayaona kwa marafiki zetu. Inawezekana yanatokea kwetu vile vile.

Nina rafiki ambaye alimuoa binti akiwa na mtoto. Baadaye akagundua kuwa mke wake na yule mzazi mwenzie wanaendelea. He has ended becoming FATAKI. Ana wake za watu na wasio wake za watu kibao.

Siri siku zote ni ngumu kuificha. Ni lazima kuwe na sababu kubwa. Ikiwa hiyo sababu ni kubwa kuliko huyo mpenzi wako, unaweza kufikiria kuwa pengine huyo si mpenzi kweli kweli.
 
Ndugu zangu, historia zilishapita, ukiuliza sana utazaa maumivu tu. Kuna jamaa yangu anajuta kujua yaliyopita coz mkewe alimtajia watu ambao wengine anajua kabisa wanawasiliana na mkewe mpaka leo,sasa haelewi wanaendeleza libeneke au vp... anakoma na maumivu sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…