Historia siku zote ni muhimu kwani historia huwa ina tabia ya kujirudia. Be careful. Kudharau historia, ni kwenda bila kujua utokako!
Binadamu siku zote huwa ni mujumuisho wa linalotokea leo, kesho, .... mpaka utakapokufa. Kila linalotokea huacha alama yake katika maisha yako na usipoangalia hayo, the chance of failure ni kubwa mno.
Tatizo ni je unauliza historia hiyo lini. Kuna mtu ameshasema hapa historia ni muhimu kabla ya commitment. Tena iwe yoote nzima nzima. Halafu ifuate comitment. Ukifanya comitment bila kujua historia, unaogelea kwenye bwawa ambalo hujui kina chake. Siku zote kuna hatari.
Tabia za watu zinajengwa na yaliyokwisha wakuta. Tujiheshimu leo, vinginevyo historia itatuhukumu. Mwanamke aliyekuwa anafanya kazi Ohio, kazi ya kujiuza, ana mtazamo fulani kuhusu mahusiano. Mtazamo ndio unaomfanya mtu awe vile alivyo. Ni muhimu kuelewa mtazamo wa mtu KABLA NA NIRUDIE TENA KABLA. Huwezi kujua mtazamo bila kujua alifanya nini huko nyuma.
Ukiwa loose leo, uwezekano wa kuwa loose mwaka ujao ni mkubwa. Hivyo kujua ni muhimu, tena ujue yoote. If you have no balls to stand them, you will have no balls to stand the relationship.