Ili historia hiyo iwe na manufaa kwako ni vema ukaifahamu (kwa kuelezwa na yeye mwenyewe au kuipata kwa njia nyinginezo) kabla hamjaamua kuoana. Kama alikuwa na mahusianao jaribu kupata ukweli ni kwa nini mahusiano hayo yalivunjika. Historia hiyo itakusaidia kumfahamu vizuri zaidi mchumba wako.Historia inaweza kutoa mwanga kuhusu tabia za mwenza wako na kukusaidia kufanya maamuzi iwapo ni mtu sahihi kuwa nae katika maisha yako kama rafiki na mwenza.
Nadhani ni hatari kujaribu kuipata historia ya mwenza wako wakati mmeshaoana tayari. Katika wakati huu historia (kama ni mbaya) itaongeza tensions badala ya kuisaidia ndoa yenu.
Cha muhimu zaidi kujua ni kwamba binaadamu tunabadilika (we are dynamic) na hivyo si vema kumuhukumu mtu kwa historia yake pekee ni lazima uzingatie ukweli uliopo sasa. Kwa mfano, kama ukiangalia historia ya mtu wakati akiwa 'teenager' na kufikiri bado ana tabia hizo wakati akiwa in his/her 30's utakuwa humtendei haki.
.........................
Wazo mbadala:
Nafahamu tunapoenda kuomba kazi waajiri mara nyingi wanazingatia uzoefu, umri, uwezo na maarifa mengine ya mtu anayeomba kazi. Sasa katika mapenzi, si vizuri pia kumpata mtu mwenye uzoefu🙂?[/QUOTE]
heshima yako mkubwa! hayo ya juu nakuunga mkono 100 kwa 99, lakini hili la chini mmhhn!!kwenye kazi sawa uzoefu sawa, kwa hili labda ungefananisha na gari...je wewe ungependa kununua gari chakavu kwa kuwa lina uzoefu wa kutembea miaka mingi na kwa muda mrefu? ile kitu nakuwa na raha unapojisi kuwa mmiliki pekee bana! japokuwa mara nyingi sio kweli, hizi presha na mashinikizo siku hizi vimezidi kutokana na kutaka kuvumbua vilivyofichika kama hivi na mawivu yasokuwa na maana! muhimu ni kutotaka kuyachunguza yaliyopita...