DOKEZO Kuna upigaji mkubwa unaendelea wa posho za kujikimu ajira mpya Halmashauri ya wilaya ya Sikonge

DOKEZO Kuna upigaji mkubwa unaendelea wa posho za kujikimu ajira mpya Halmashauri ya wilaya ya Sikonge

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna upigaji mkubwa unaendelea wa posho za kujikimu ajira mpya halmashauri ya wilaya ya Sikonge.

1. Katibu mkuu aliwandikia barua halmashauri zote zenye maelekezo maalumu kwa ajili ya fedha za kujikimu na barua hiyo ilielekeza bayana kuwa watumishi wa ajira mpya kwanzia Januari 2025 hadi Aprili 2026 wawe wamelipwa posho za za kujikimu na ripoti irudishwe kabla au tarehe 15/06/2026

2. Lakini cha ajabu watumishi wa ajira mpya hasa idara ya afya kila tukiuliza stakihi zetu ni maelezo tu ambayo hayaeleweki mara wanatoa sababu kuwa tujaze vendor forms ilihali tulizijaza wakati wa kuripoti mambo haya yanaashiria kuwa kuna viashiria vya upigaji na wizi wa fedha za kujikimu kwa masilahi yao binafsi

3. Tunaomba wizara ya tamikufyatilia hili kwani wanaweza kuwa wamewaandikia barua na ripoti kuwa tumeshakwisha pokea fedha hizo lakini si kweli na tunaomba waliohusika wachukuliwa hatua kali za kisheria kwa udanganyifu kwani ni kinyume na sheria za utumishi wa umma
 

Attachments

Back
Top Bottom