DOKEZO Kuna utoroshaji Madini huko Lemshuku, Manyara

DOKEZO Kuna utoroshaji Madini huko Lemshuku, Manyara

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu andaa hela twende Dubai connection ipo. Kama huna ujuzi utafute ndani ya mwaka huu, mwaka kesho panapo majaliwa tuondoke. Tukifika huko tunapiga mishe huku tukicheki utaratibu wa kusonga mbele kama Canada ama Marekani. Hii Tanzania ni ngumu sana aisee!
Mkuu ukipata connection ya kusepa usiniache, nishapack kila kitu.
 
Mkuu andaa hela twende Dubai connection ipo. Kama huna ujuzi utafute ndani ya mwaka huu, mwaka kesho panapo majaliwa tuondoke. Tukifika huko tunapiga mishe huku tukicheki utaratibu wa kusonga mbele kama Canada ama Marekani. Hii Tanzania ni ngumu sana aisee!
Nakupigia tuongee vizuri jamaa yangu.
 
Kuna meneja (Zulfika Abdulkarim) wa mgodi moja wa madini ya Vito Lemshuku, Wilayani SIMANJIRO, yanayoitwa green garnet ametorosha madini ambayo thamani yake haijajulikana Kati ya tar 15 Machi hadi tar 22 Machi 2024, lakini baada ya Wizara kupata taarifa walikuja kuhoji wafanyakazi wakamchukua huyo meneja mara mbili mfululizo kana kwamba alikuwa analazwa sero matokeo yake akawahonga maafisa madini hiyo kesi ikaisha juu kwa juu.

Kibaya zaidi kuna madini yalizalishwa kabla ya hapo yakakaa kule Mererani zaidi ya miezi 2 bila kuthaminishwa.

Sasa, hilo tukio la upotevu wa madini likampa huyo meneja ukaribu na watu wa wizara halafu baada ya wafanya kazi kudai yale madini kufanyiwa tathmini ndipo ukafanyika udanganyifu kwenye uthaminishaji ambao ulihusisha hao maafisa madini (hasa Mathias Malebo Paul), huyo meneja (Zulfika Abdulkarim) na mwenye mgodi.

Mwanzo, meneja alikuja kusema yale madini thamani yake ni milioni 6 na laki tano, makubaliano wafanyakazi watapewa asilimia 10% ya thamani ya madini ambapo tungegawana laki 6 na elfu 50 kwa watu 12 ambapo kila mtu angepata mgawo wa elfu 54,000 hivi, akasema imeonekana hiyo hela ni ndogo tajiri akaongeza kila mtu apewe laki 150,000.

Kiuhalisia yale madini thamani yake sio 6,500,000/= green garnet ni bei ghali gram 1 ikiwa safi na nzuri yenye rangi nzuri inauzwa mpaka milioni 3 kwa gram 1 tena hiyo ni minimum, sasa ule mzigo ulikuwa unajaa chepe au kisahani kidogo, so haiwezi kuwa milioni 6 na nusu.

Baada ya wafanyakazi kuhoji na kutaka kuona risiti ya uthaminishaji madini ndipo huyo meneja akatusomea risiti ya malipo ya Kodi iliyolipwa serikalini, hapo mimi nikagundua kuwa hiyo milioni 6 na nusu haikuwa thamani halisi ya madini tuliyozalisha bali ilikuwa Kodi iliyolipwa serikalini, nikaamua kufatilia Wizarani kule Mererani.

Afisa moja mthaminisha madini (Mathias) akaendelea kusimamia kuwa yale madini thamani yake ni milioni 6 na nusu, lakini baada ya mwenzetu kugoma na kuweka hoja nzito kuwa ataenda kulalamika TAKUKURU ndipo R.M.O (Regional Mineral Officer) akatoa document ya uthaminishaji hayo madini ikawa inaonekana thamani ya hayo madini ilikuwa milioni 89,566,000/= milioni 89 laki 5 na machenchi. Kwa mantiki hiyo, mgawo wetu kama wafanyakazi utakuwa 10% ya 89,566,000 ambayo ni sawa na milioni 8 na laki 9 hivi. Kwa mgawo, kila mtu angepata milioni 1 na laki 1 na chenchi, hata hivo alidanganya kuhusu idadi ya wafanyakazi sio 12 tulikuwa 9.

Ufuatiliaji huo ulisababisha huyo meneja akamfukuza kazi mwenzetu, hadi sasa kazini hayupo tena mwezi 1 umepita. Watu hawajalipwa stahiki zao wamebaki kutishwa kufukuzwa kazi.

Serikali imekosa mapato mengi sana maana ule mzigo thamani yake halisi yaweza kufika zaidi ya milioni Mia sita (Tsh 600,000,000/= maana ile milioni 89 ni kiasi minimum walichokubaliana kuandika kuwa thamani ya mzigo baada ya tajiri kuwahonga hao maafisa.

Mimi naomba TAKUKURU ifanye uchunguzi wa kushtukiza. Wafanyakazi bado wapo wahojiwe, watasema ukweli na pia mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wadogo (MAREMA) Mzee Swalehe alipewa nakala ya thamani ya hayo madini na R.M.O na bado hakuna kilichofanyika. Madai ya wafanyakazi yamepuuzwa. Huu ni uovu wa hali ya juu na pia ni kuhujumu jasho za watu na uchumi wa nchi yetu.

TAKUKURU wakitaka ushahidi, nipo tayari kuwapa ushirikiano. Naomba huyo meneja na wahusika wengine wachukuliwe hatua.

Uzuri ni kwamba pale Mererani TAKUKURU wakiamua kufanya uchunguzi waangalie CCTV camera hayo madini yataonekana jinsi yalivyokuwa na kiasi chake.

View attachment 2999548

Hii picha ni aina hiyo ya madini ya vito yanaitwa "Green Garnet" na huo mgodi unaitwa kwa MWARABU eneo la LEMSHUKU wilaya ya SIMANJIRO, MANYARA.
Naomba kumjua huyu mathias malebo paul yukoje?

Nina sababu,nimjue kama ni yeye ninayemfahamu tuseme tu serikali haiko makini kuajiri watumishi wa umma.
 
Hicho kidole chako hako kaalama kwenye kucha sio kageni nishakaona hapa ofisini, nazani nikikuona ntakukumbuka sura yako.
 
Hili ni Tatizo la watumishi wa umma wengi Nchi hii wakipata fursa hawataki mchezo kabisa. Ni wezi Kuliko wezi wa huku Mtaani
Wakiangalia baadhi ya viongozi wao ni wezi vile vile, probably huwa wakisema wanafukuzwa na moyo unavunjikia hapo hapo
 
Hata umkamate mwizi wa madini hakuna kitu kitafanyika wao wanajua nani wa kumuona ili mambo yaende sawa..Nchi ngumu hii
 
Ila kuwazulumu wachimbaji huo ni ushetani wa hali ya juu..hao watu wanarisk maisha yao..jasho linawatoka kila siku..embu tuwe na ubinadamu na hofu ya Mungu.
 
Ila kuwazulumu wachimbaji huo ni ushetani wa hali ya juu..hao watu wanarisk maisha yao..jasho linawatoka kila siku..embu tuwe na ubinadamu na hofu ya Mungu.
Hapo walifanya kosa kubwa. Kuwadhulumu watu wanaojua mchongo mzima ni ujinga wa hali ya juu na tamaa za hovyo.
 
Umebarikiwa sana Nyikani ila watu wako waliorogwa walale USINGIZI,

Ni wakati wa kuamshwa sasa,

Imagine madini hayo 1gram =3ml tzshs. Wakati gold 1gram haizidi laki 2na nusu😳
 
Ulivyosema mwarabu basi nikakata tamaa kabisa. Waliosoma Cuba wananielewa
 
Back
Top Bottom