Zero Competition
JF-Expert Member
- Sep 12, 2018
- 347
- 553
Nimekua nikiona washauri wengi wa masuala ya mahusiano wakitushauri wanaume kuoa wanawake bikra kwa kigezo kwamba ndio wanawake pekee ambao hawawezi chepuka kwenye ndoa zao tofauti na wale ambao wanaingia kwenye ndoa wakati tayari bikra zao zlishatolewa na wanaume wengine.
Hao wanaotushauri tuoe wanawake bikra usikute hata wao wenyewe wameoa wanawake ambao walishatolewa bikra na watu wengine ola hawawezi kusema ukweli.
Hakuna kitu kigumu kama kupata mwanamke ambae hajawahi fanya mapenzi na mwanaume mwingine katika karne hii ya utandawazi. Wasichana wengi siku hizi wanajiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi hata kabla hawajafikisha miaka 18 na wanajua staili zote za kufanya mapenzi kuliko hata watu wazima.
Kule kwa wala urojo tunasikia wanawake wanaolewa wakiwa na bikra zao ila bikra ya Sodoma na Gomora wanakua walishatolewa kitaaaambo. Mimi huwa nashangaa sana nikiona mtu anamshauri mwenzake kwamba aoe msichana bikra wakati bikra zenyewe zimekua adimu.
Siku hizi kwenye kundi la mabinti 50 unakuta mmoja tu au wawili ndo wenyewe bikra na wakati mwingine usipate hata mmoja mwenye bikra katika hao wasichana 50.
Ni sawa inawezekana ukawa na bahati ukapata mwenye bikra ila bado hakuna uhakika wa 100% wa kila mwanaume kupata mwanamke bikra, unaweza kumpata ambae hajatumika sana ila kupata bikra kabisa ni ngumu sana.
Binafsi sina imani kwamba ukioa bikra ndo atatulia kwenye ndoa yake, wapo waliolewa wakiwa bikra na mwishowe wamechepuka kama kawaida. Kuchepuka au kutochepukanni tabia tu ta mtu binafsi na pia malezi ya wazazi yana mchango mkubwa sana katika kumuandaa binti anaetarajia siku moja kuingia kwenye maisha ya ndoa.
Upi mtazamo wako juu ya kuoa mwanamke bikra ?