Kuna uwezekano wa kuhoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mahakamani?

Kuna uwezekano wa kuhoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mahakamani?

clearmind

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
813
Reaction score
1,913
Narudi nyumbani baada ya Hustles za hapa na pale. Naombeni wenye uelewa kuhusu Hili jambo mnifahamishe. Je, Kuna uwezekano wa KUHOJI uhalali wa MUUNGANO WA TANGANYIKA na ZANZIBAR MAHAKAMANI?
 
Kwani hakuna Zanzibar na wazanzibar ??
Hawana nchi yao na serikali yao ??
Katiba yao ndio msingi wa kujibagua
Hakuna mtanganyika mbaguzi bali ni wazanzibar ndio wanajibagua kwa kila kitu kwa mujibu wa katiba yao wenyewe,SOMENI KATIBA YA ZANZIBAR MUONE WAO WANAVYOJIBAGUA KUTOKA TANZANIA.
 
Wao ni wazanzibar daima dumu
Wao wanajiita wazanzibar
Wana serikali yao
Wana nchi yao
Wana kila kitu chao
Wana vitambulisho vyao
Wanajitambulisha kama wazanzibar kokote duniani
Ni wakati kula RASILIMALI ZA TANGANYIKA PEKEE NDIO WANAJIITA WATANZANIA WAKISHIBA wanaendelea kujitambulisha kama Wazanzibar
 
Ni wakati wa kuamka na kuliangalia Hili suala Tena katika vyombo vya Sheria.
 
Narudi nyumbani baada ya Hustles za hapa na pale. Naombeni wenye uelewa kuhusu Hili jambo mnifahamishe. Je, Kuna uwezekano wa KUHOJI uhalali wa MUUNGANO WA TANGANYIKA na ZANZIBAR MAHAKAMANI?
Kuna ukweli tunatotakiwa kuufafanua na kama ni kero irekebishwe kama kweli tunafikiri muungano huu ni wa muhimu.

1. Wazanzibar wengi sana wanamiliki ardhi na majengo bara, kama raia. ila Wabara wanachukiwa wakienda kule, wanaitwa chogo, na katiba yao inazuia watu wa bara kumiliki ardhi. Juzi nilikuwa Dodoma, kwenda benjamin Mkapa kwenye kona ya Udom, kuna migorofa fulani hivi imejengwa, wanasema karibu na vile vijengo vya majaji, wengine wanamtaja mzanzibari fulani anamiliki hiyo migorofa. tukisema wazanzibar leo hii muungano umevunjika waondoke, wengi wataanza kuuza nyumba nyingi na ardhi kubwa wanayoimiliki. KWANINI BARA HATURUHUSIWI KUMILIKI KULE? faida yao ni nini?

2. kwenye ajira, hii ni kero, wazanzibar maelfu na maelfu wameajiriwa bara, hata kwenye mambo yasiyo ya muungano, wameajiriwa bara ambayo kiukweli ipo bara kwasababu zanzibar kuna utawala wao, lakini wabara hawaruhusiwi kabisa kuajiriwa zanzibaar, hii ni kero, inatakiwa iondolewe, ama la kila mtu abaki kwake.

3. wazanzibar wanakuwa wabunge kule kwao, na huku. akiwa mbunge kule kwao, atakula masurufu ya kule na atakuja kula masurufu ya bara kwa kodi za watu wa bara. tuambieni, yale mipesa wanaku wabunge 50 wa zanzibar wanakiula, zanzibar huwa imechangia bei gani? ni pesa za walipa kodi wa bara. na hao hao wakifika huku wakishiba, wanasenma twende kule kwa passport, kwa msiojua, kile ameongea yule mbunge wa zanzibar kwamba wabara twende kwa passport kwao ndicho kilichopo kwenye mioyo ya wazanzibari wote hata wenye mamlaka huku na hata walioajiriwa huku na hata wanaomiliki ardhi huku, amesema kilichopo kwenye mioyo ya wengi. wala hatakiwi kulaumiwa. kwa waliofika zanzibar wanajua kuwa hicho ndio huwa matamanio yao.

4. mzanzibar anaweza kuwa Mkuu wa wilaya, mkoa, na waziri bara, ila sisi kule marufuku. kwanini?

nimeongea hayo kwa uchache tu, lakini ukweli mwingi hata wanaopinga wanaujua, kama tunataka muungano uwepo, ondoeni kero hizi kwa watu wa bara, ama la, kila mtu achukue hamsini zake kwasababu hakuna kitu wabara wanafaidika nacho as of now. na hawajawahi kufaidika. watu wasioelewa watasema huu ni uchochezi, ila jibuni kwa hoja kama mnazo.
 
Back
Top Bottom