Naongezea; Unafiki ni hali ya mtu kutenda tofauti na maneno anayoyasema siku zote. Yaani unahubiri hiki, lakini unatenda kile!
Kwa mfano, unasema: "Rushwa ni mbaya sana" lakini ukienda pembeni unaomba rushwa.
Ni kweli, inawezekana Tanzania unafiki upo. Kwa mfano; Bwana yule alikuwa anapenda kusema maendeleo hayana vyama, lakini ilipofika kwenye uchaguzi wapinzani wakaenguliwa.
Kwa hoja hizi (Corona, Makinikia, Kesi za kisiasa, Mapato na matumizi), tunaweza kusema wasaidizi hawakuwa wanafiki, bali ni njaa na kumwogopa Jiwe. Rejea yule bwana msajili wa hazina, alipompinga Jiwe, ni nini kilitokea.