JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Wakati ambao zimekuwa zikiripotiwa taarifa za uwepo wa ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo mbalimbali nchini lakini inashangaza bado inashuhudiwa uwepo wa masuala ambayo yanaweza kuchangia na kuweka hatarini watu kupatwa na magonjwa ya aina hiyo bila kuchukua tahadhari.
Inasikitisha kama sio kuleta mshangao, kumekuwepo na uzembe kwa baadhi kampuni ambazo zimepewa tenda ya kuzoa taka Jijini Dar es Salaam hata maeneo mengine nchini kutozingatia usalama wa wafanyakazi wao wakati wanapokuwa wanatekeleza majukumu ya kuzoa taka.
Imekuwa ikishuhudiwa baadhi ya wafanyakazi baadhi ya makampuni ya kuzoa taka bila kuwa na dhana maalumu za kuwakinga na madhara yanayoweza kuwapata katika mchakato wa kuzoa taka hizo, mfano kuna wakati unakuta Mtu anabeba taka kwa mikono kupakia kwenye gari bila kuvaa chochote cha kumkinga.
Kwa mara kadhaa hali hii nimekuwa nikikutana nayo hasa kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, ukizungumza na wahusika wanadai wameshazoea kufanya hivyo. Binafsi uwa nabakia kujiuliza Watu hao likijitokeza janga la kipindupindu wanaponeaje!
Lakini mfano mwingine katika mazingira ya aina hiyo, kuna jambo lingine limekuwa kama rasmi, unakuta vijana wanaobeba taka wamekaa juu ya taka kwenye magari huku yakiwa kwenye mwendo bila kuwa na dhana maalumu za kuwakinga na madhara ikiwemo harufu mbaya inayotokana uchafu huku pia suala hilo likisaulika mithiri ya kwamba haliwezi kuleta madhara ya kuhatarisha usalama wao.
Hata hivyo najaribu kufikiri hizo kampuni hawajipi wenyewe tenda, je, wanaotoa hizo tenda hawatoi masharti kwa kampuni kuzingatia usalama wa wafanyakazi, kwamba kama waombaji wa vibali hawakidhi kigezo hicho wasipewe tenda! au kuna mazingira ya rushwa na kujuana ambayo yatoa mwanya wa kutowajibishana?Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) nao wako wapi, au hilo suala wanaliona dogo hawaliwahusu.
Uenda kutokana na uhaba wa ajira hasa kwa vijana linaweza lisiwe jambo la kushangaza kuwaona wakijitojeza kufanya kazi hizo katika mazingira ambayo hata hayazingatii usalama wao labda ndio linawapa kiburi waajiri, lakani hilo lisiwe sababu ya haki zao kusiginwa mchana kweupe, tunazo mamlaka ambazo zimepewa jukumu la kulinda haki hizo muhimu wanatakiwa kusimamia kidete hilo na kama wanashindwa kutokana na uzembe hawana sababu za kuwepo kwenye Ofisi za Umma.
Sanjari na hilo lakini ni vyema kampuni ambazo zinashindwa kuzingatia umuhimu wa suala hilo kwa kuhatarisha afya za wafanyakazi wao wawajibishwe kutokana na uzumbe kwa kuwa wanawaweka wafanyakazi katika hatari ya kupatwa na magonjwa kama kipindupindu ambao umekuwa ukitajwa kutokana na mazingira ya uchafu.