Kuna Vibaka nawaona kabisa wanakula Rada Dirisha la Gheto langu, tafadhalini nichagulieni Adhabu ya kuwapa ambayo hawatoisahau Milele

Kuna Vibaka nawaona kabisa wanakula Rada Dirisha la Gheto langu, tafadhalini nichagulieni Adhabu ya kuwapa ambayo hawatoisahau Milele

Pepper spray ndio dawa yao kisha unainamisha mmoja baada ya mwingine.
Kwa kifupi mwizi yeyote ana elements za kishoga kupenda vitu vya watu bure bure..!
Inamisha wangese hao..))
 
NIMEKUMBUKA KISA CHA KWELI CHA JIRANI[emoji23]


Kuna mzee mmoja askari magereza alivamiwa na wezi na walitaka kumuiibia mifugo yake.

Mzee kucheki dirishani anaona vijana 4 akaona siyo kweli nkitoka nje naweza nkapigwa mimi na hawa wezi.

Akaamua atumie trick ya Cuba akaenda chini ya kitanda akaokota panga lake akasogea mpka dirishani na kuanza kulinoa panga taratibu akiwa ndani ya nyumba.

Wezi wakastuka katika harakati za kusikilizia kama mwamba atafanya nini tena, wakasikia mzee anamwambia mke wake kwa sauti kubwa kuwa “NITUNZIE WATOTO WANGU VIZURI NA NIOMBEE MUNGU APOKEE ROHO YANGU KWAMAANA NAENDA KUFA NA HAWA WEZI”

[emoji23][emoji23]
Wale was.enge walichimba dakika hiyhiyo
 
Je,

1. Wakija Kuniibia nimsaidie Kazi Israeli ili wakayaanze Maisha yao mapya Kinondoni au Kisutu?

2. Wakija Kuniibia niwe tu Mpole wachukue watakacho

3. Wakija Kuniibia nivizie wa Kwanza kuingiza / kupenyeza Kichwa chake Dirishani Kwangu na nikitenganishe Kichwa chake na Kiwiliwili?

4. Wakija Kuniibia nimtegemee tu Mungu wangu wa Kanisa Katoliki au nimwage Maji ya Mtume Mwamposa Chumbani Kwangu?

5. Wakija Kuniibia niweke CD yenye Mlio wa Risasi na niiseti iwe inajirudia kila baada ya dakika 15 ili Kuwatisha?

6. Wakija Kuniibia nitegeshe Flat Screen yangu iliyochoka kama DalaDala za Vikindu Dirishani kisha kwa Makusudi niweke Mkanda wa Mibaiolojiano / Mibanduano ili iwatamanishe na Wategeshe Mimacho yao kisha nitoke nje taratibu nikawashtue Majirani na tuje Kuwadaka kiurahisi na tuwapige Usiku Kucha hadi IGP Mwetu ( Poti ) Mzanaki Mwenzangu Wambura atakapokuja Kumuokoa na Police wake?

7. Wakija Kuniibia kwa Makusudi niwashe Taa na nijifanye nafanya Mazoezi ya Karate huku nalia Kikarateka kama Muasisi Bruce Lee na muda mwingine niwe napiga Sarakasi za Miguu juu Ukutani na nimalizie kwa Kucheza na Panga huku nikiliburuza Sakafuni Kiukakamavu na nikimaliza nijifanye naongea na Simu na Mwanajeshi wa Lugalo King Kong III nikimuulizia Bunduki yangu ameiacha na Risasi ngapi kwani nataka kuanza Zoezi langu tukuka la Kulenga Shabaha kwa Usiku huu?

Nayasubiri majibu yenu kwani bado nawaona wanapitapita Kimkakati usawa wa Dirisha langu hivyo nami nataka kuwaonyesha kuwa Mimi ni Mtoto wa Mjini kuliko Bujibuji Simba Nyamaume, Bila bila na adriz

Sema nini popoma…!!
Ni vile nimechelewa kuja hapa!
Ila namba 7 imekaa poa mkatoliki mwenzangu, tofauti ni kuwa wewe hujuo kupiga kinanda wala kusoma nota!
Kesho uje ibada ya sa nne unione navyobonya pedal, na utabarikiwa sana na sebene la shukrani ambalo ni utunzi wangu kabisa, nilioumiza kichwa kwa zaidi ya mwezi!
 
Back
Top Bottom