KERO Kuna vijana katika Stendi ya Daladala Mbezi Mwisho huwazuia watu wanaoingia kwa magari au pikipiki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna kundi la vijana katika Stendi ya Daladala Mbezi Mwisho ambao huwazuia watu wanaoingia kwa magari au pikipiki binafsi kuwapeleka abiria wanaosafiri.

Vijana hao, ambao hawana utambulisho rasmi, hujifanya kuwa askari na wanapokamata chombo, hasa pikipiki, hukisogeza eneo la vyoo. Baadaye humtaka mhusika kulipa kati ya TSh 10,000 na 20,000. Malipo hayo hayapewi risiti ya Serikali, jambo linalozua wasiwasi kuhusu matumizi ya fedha hizo na mamlaka ya kundi hilo katika eneo hilo.

Naomba Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Adv. Msando, pamoja na timu yake, wafanye uchunguzi wa kina kuhusu kinachofanyika katika stendi hiyo, ikiwemo madai ya tozo zisizo rasmi na uwezekano wa Serikali kukosa mapato.

Wito wangu ni kwa mamlaka kuweka utaratibu rasmi unaoruhusu watu binafsi kuwapeleka abiria katika stendi hiyo na, inapohitajika, chombo husika kitozwe ushuru kwa utaratibu unaotambulika na Serikali na kupewa risiti. Hatua hiyo pia itasaidia kuondoa hofu miongoni mwa wananchi wanaotumia eneo hilo.
 
Itakuwa wanakula na wake maaskari kunakituo hapo pembeni kabisa upande magari yanapoingia
 
Hapo usijisumbue viranja wao ni askari wanaokuwa humohumo stend
 
Sijaelewa... Wanazuia na kumamata magari yanayoingia stand?
 
Mmmh, wanakamata vipi magari yanayoingia stand ndogo?
Hii naisikia kwako, stand ndogo na hata kule Magufuli, watu wanaingiza magari na kulipa tozo ya 1,000 kwa stand ndogo, kule Magufuli wanalipa 500 wanapewa risiti kabisa.
 
Jichanganye uingie na boda boda jioni ukiwa ready na abiria uone
 
Mmmh, wanakamata vipi magari yanayoingia stand ndogo?
Hii naisikia kwako, stand ndogo na hata kule Magufuli, watu wanaingiza magari na kulipa tozo ya 1,000 kwa stand ndogo, kule Magufuli wanalipa 500 wanapewa risiti kabisa.
Pale stendi ya daladala jichanganye uingie sasa hasa pikipiki
 
Pikipiki haziruhusiwi, ila private cars zinaruhusiwa na wanalipia kabisa 1,000 ushuru kama wanavyofanya daladala mkuu.
 
Back
Top Bottom