Kuna viongozi hawana uelewa wa katiba, sheria, kanuni, na taratibu. Elimu iendelee kutolewa, na kila mmoja amfundishe mwenzake

Kuna viongozi hawana uelewa wa katiba, sheria, kanuni, na taratibu. Elimu iendelee kutolewa, na kila mmoja amfundishe mwenzake

Joined
Jul 6, 2024
Posts
97
Reaction score
72
Kuna baadhi ya viongozi wana vyeo ila hawazijui katiba, sheria za nchi, kanuni, miongozo, na taratibu. Elimu iendelee kutolewa, na kila mwenye kujua jambo amfundishe mwenzake.

Tusome Katiba ya CCM 1977, Toleo 2022, Uk. 02, Ibara ya 05(04). Wanachama wa CCM tunasisitizwa kusimamia utekelezaji wa siasa ya CCM pamoja na kuendeleza fikra za viongozi waasisi wa vyama vya TANU na ASP, kama zilivyofafanuliwa katika maandiko mbalimbali ya vyama hivyo. Mheshimiwa Mohammad Mchengerwa, Waziri wa TAMISEMI, tarehe 09/11/2024 alisema: "Baba wa Taifa (Mwl. Julius Kambarage Nyerere) alizungumza sana katika hotuba zake kuhusu elimu, na eneo hili Rais wa Awamu ya Sita amejikita kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu." Mwisho wa kunukuu.

Tusome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, Toleo 2005, Ibara 34(4) Uk. 33 na Uk. 34, Ibara ya 35(1). Katiba ya CCM 1977, Toleo 2022, Uk. 10-11, Ibara ya 15(3)(6)(7) inatufundisha wajibu wa Mwanachama wa CCM kujitolea kuondosha ujinga kwa kujielimisha kadiri ya uwezo wake na kutumia elimu yake kwa faida ya watu wote, huku akiwa tayari kujikosoa na kukosolewa ili kuwa na msimamo sahihi wa CCM.

Ibara ya 05(09) na 05(11) ya Katiba ya CCM 1977, Toleo 2022, inakubaliana na utawala wa sheria na kutambua Tangazo la Haki za Binadamu. Ibara ya 05(14) inasisitiza jitihada ziendelee za kuuondoa ujinga. Ilani ya CCM 2020-2025 inatukataza kufanya kazi kwa mazoea. Tukiyatimiza haya kwa ukamilifu tunajiepusha na kuvunja sheria ya nchi, "The Political Parties Act, Chapter 258," inayotutaka kutii na kufuata maandiko ya chama kwa ukamilifu wake.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, Toleo 2005, Ibara ya 26(1), Uk. 27 inatueleza kuwa kila mtu ana wajibu wa kufuata na kuitii katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano. Ibara ya 09(b) inaeleza kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa. Mwisho wa kunukuu.

Shekhe Othman Khamis Juma, Kaimu Imamu wa Masjid Mtoro, akiwa Masjid Maamur tarehe 30/09/2024 alisema: "Mtume (Muhammad SAW) kasema, mkifungua midomo kuzungumza, semeni kweli. Mtu yeyote anayetaka baraka kwenye dunia hii si ni kumwamini Mungu na kumuogopa!" Hapa kila mmoja alinde ulimi wake na asiseme uongo; usitoke mdomoni mwako uongo. Mwisho wa kunukuu.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, Toleo 2005, Uk. 13, paragraph ya kwanza inatueleza: "Kwa kuwa sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu, na amani." Mwisho wa kunukuu.

Tusome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, Toleo 2005, Uk. 20, Ibara ya 13(1) inatueleza kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ubaguzi wowote kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria. Mwisho wa kunukuu.

Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, tarehe 12/11/2024, akiongea na wanahabari alisema: "Tukiendekeza ukali, tujuwe tunadumaza uhuru wa watu kutoa maoni yao, na mwisho wa saa haina faida yoyote kwa nchi yetu." Mwisho wa kunukuu.
 
Mwandiko mbaya. Mambo ya kucopy toka kwenye pdf.
 
Back
Top Bottom