Kuna viongozi walipanga kuingia nyumba za ibada na vyeo vya jana mchana ila asubuhi waliposoma mkeka hata ibadani wamesusa

Kuna viongozi walipanga kuingia nyumba za ibada na vyeo vya jana mchana ila asubuhi waliposoma mkeka hata ibadani wamesusa

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Hakuna jambo la kibabe alilofanya mama kama kuharibia watu mwaliko wa Pasaka.

Kuna watu wamegoma kwenda kanisani kwa sababu title zao zimebadilika au hazipo tena.

Wengine walitamani madereva wawapeleke sehemu ila wanaamini wao sio mabosi wa hao madereva tena. Wapo waliowaalika wananchi na familia kwa mkuu wa mkoa au wilaya ila asubuhi wanabaini wao siyo wakuu wa wilaya, siyo mawaziri wala makatibu wakuu tena

Hii hali naifananisha na kifo, usipojiandaa na kumkabidhi Mungu Maisha yako kikifika unaondoka. Usipokanidhi magari ya serikali saa tisa na nusu utalazimishwa kuyakabidhi ukiwa usingizini.

Lakini pia, Busara ilipaswa kumwambia mama hawa watu wana ratiba yakutoa salam za pasaka wavumilie hadi misa ziishe. Ila ndio vile tena. Acheni familia ziishe kwenye nyumba zenu kuepuka aibu yakutimuliwa siku sikukuuu.

Je siku ya Eid nayo itavutugwa au hali itakuwa shwari?
 
Hayo ni mambo ya kawaida tu katika haya mavyeo ya kuteuliwa. Na ndiyo maana wakiteuliwa wanaiba haraka haraka na kujitajirisha ili msala kama huu ukija uwakute wako vizuri. Trust me wote hawa tayari wako vizuri sana kiuchumi. Na wengine wakitulia na kuchapa kazi unaweza kuwakuta wanarudishwa tena. Ukishaingia kwenye system ya CCM basi umeula!
 
Na wale Jamaa wa GSM nao naona Iddi El Fitri yao imefika mapema kabla ya wakati.

Bashe nae atafuturu kwa Balimi mimi mwenyewe hapa nilipo nimekaa na Bia yangu niipendayo Guinness Black Power.🤤
 
Bia za pasaka zimenoga japo tupo dar ila kibaridi kimekua kama cha chuga
 
Back
Top Bottom