Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Gharama kubwa za kodi za wananchi zimetumika. Lakini wapo viongozi ambao wametumia ofisi za umma kukwamisha miradi ya SGR kwa malumbano yasiyo na tija.
Ukijiuliza wananufaike utasikia wanamiliki mabasi na malori ya mizigo na hivyo miradi hii inakuja kuwaondolea abiria na mizigo. Lakini pia wanaambatanisha hujuma zao na kauli kwamba wana mikopo ambayo endapo SGR itakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma basi watashindwa kulipa mikopo yao.
Watu hawa wana nguvu sana, wamekwenda kwa watumishi wa umma na kuwatengenezea hofu wasiruhusu kazi kufanyika kwa kasi inayotakiwa.. Wamemega hata baadhi ya fedha za fidia wananchi walipwe fidia kidogo lengo ni wao kugombanisha serikali na wananchi. Mfano mzuri ni fidia eneo la tabora , mtu analipwa fidia laki mbili na hakuna kuhoji.
Niombe watumishi wa umma watambue Mhe. Rais anaona wanavyomkwamisha. Siku si nyingi makatibu wakuu wataondolewa ofisini, na hata wanasiasa mawaziri wataondolewa ofisini kwa kukwamisha miradi hii.
Kama serikali ilijua hakuna fedha kwanini waliingia mikataba hadi Mwanza badala ya kukamilisha miradi ya awali? Au ndio kusambaza rasilimali kazi ya mwaka ifanyike miaka kumi? Tuweni wazalendo pls