Kuna vita vimeibuka kati ya mama yangu mzazi na mke wangu

Kuna vita vimeibuka kati ya mama yangu mzazi na mke wangu

Ishi kama kunguni, ukikaa na mama umauma na kupuliza. Ukikaa na mama watoto unauma na kupuliza

Unaishi kama chawa pro max. Especially ukijua mama mgomvi

Mfano unamnunulia mama kazawadi unampa mkeo asijue. Unampa mkeo zawadi mama asijue, ....

Kifupi unatakiwa uwe kubwa jinga
 
Kuna mambo unapaswa kujua mapema tangu unapo oa.

Mama ni mama na anayonafasi yake iheshimiwe na wote.

Mke ni mke wako na aheshimiwe na wote ikiwa ni pamoja na mama na dada zako.

Pili mama akija kwako anapaswa kutambua yeye ni mengi wenu na ataheshimiwa. Lakini Hana mamlaka yeyote je ya wakazi wa familia hiyo.

Mkienda kwa Mama nyie ni wageni wake hamna lolote mnaweza Amina maana sio kwenu.

"Mume ataacha familia....... na kuambatana na mkewe...." Maana yake nyie mnakaenu.

Ugomvi inaanza pale mmoja wenu anapohisi anamamlaka juu ya wengine ingali yeye ni mgeni.

Huyo aambiwe TU hata kama anayohaki ya kusema alipaswa kutafuta platform sahihi. Nje ya hapo lazima ugomvi.
 
Msaada

Kuna vita vimeibuka kati ya mama yangu mzazi na mke wangu!! Ninafanyaje ndg zangu, ninashindwa kumjadili mamangu kwa kumkosoa mbele ya mke wangu.!!

NB: mama anaishi kwake na mimi naishi kwangu na mke wangu
Kaa na mkeo na mamaako pia km hawaelewani we nunua tu cd ya kuchambana na uweke kwa zamu.
Alafu walisema kataa ndoa ukae na mama tatizo we hukuja kikaoni.
 
Bila shaka unamuelewa vizuri mama yako hulka zake na pia unamuelewa vizuri mke wako hulka zake, hii itakusaidia kuelewa ni yupi kati yao mwenye tatizo kwa mwenzake. mama mwenye hekima hawezi kuanza ugomvi na mkwewe na mke mwenye hekima hawezi kuanza ugomvi na mkwewe hata kama amekosewa. Kiufupi ni kwamba mama yako na mke wako wote wana mihemko na hawana hekima, make sure hukai upande mmoja
 
Nani kakufahamisha kuna vita/ama umeiona wewe mwenyewe?
Umejaribu kujua tatizo liko wapi?
Kama ni mama tumia busara,kama unaishi nae mrudishe kwake,

Kama ni mke apewe onyo kali mana ni kukosa adabu kuwa na vita na mkwe wake.
 
Ukitaka familia yako iwe salama na mahusiano yako na mama yako yawe salama fanya hivi.

Delegation of power

Jitahidi ugawanye madaraka kati ya mke wako na mama yako .

Kwasababu hapo kinachogambania ni hiyo power

So mama anataka kuwa na sauti juu yako na mke wako anataka kuwa na sauti juu yako.

Hivyo wewe wagawanyie madaraka ili wajue chochote unachompa mama au mke ni kwasababu umependa na sio kwa influence ya yeyote.
 
Kama umeoa sista du, tatizo linaanzia hapo. Mama anaona pigo za mkeo sizo thus anajaribu kumuignore the same to Mke. Chamsingi simama kama gentleman usiegemee upande wowote ipo siku yataisha tu
 
Hii thread mbona haileweki?

Ushauri ni acha ufala na simama kama mwanaume. Koromea hiyo mbuzi yako mwambie kuanzia leo ni marufuku kuongea kuhusu mama yako. Na mwambie mama yako aache kuongea kuhusu mkeo. Kama mama yako ni wale wanaojitambua na sio micharuko ya Kiswahili basi mueleweshe kiustaarabu.

Either way wewe ndio mwenye maamuzi lakini inaonekana hujui wajibu wako kama mwanaume mbele ya wanawake. Bila shaka utakuwa umelelewa na single mother bila ya baba kama role model. Sababu hilo sio tatizo in the first place. Mimi sioni tatizo lolote zaidi ya drama za kike tu.

Do your damn duty!
 
Back
Top Bottom