Kuna vita ya kikoo kwa sasa inaendelea Tarime kimya kimya, baina ya koo ya Wanchari na Wakira.
Kinachogombaniwa hapa ni mashamba mipakani mwa vijiji vyao.
mgogoro huu unasababishwa na tajiri mmoja ambaye anakodisha mashamba ya koo nyingine kwa nguvu huku akidhamini vijana kutoka sehemu nyingine za tarime kupigana ili eneo hilo libaki milki yake.
Vijana wa vijiji hivi wakiwa chini ya viongozi wa kimila na koo zao wanakutana mipakani wakiwa wamejihami na mapanga, mikuki na mishale huku kila upande ukishambulia upande mwingine ana kwa ana , au kwa kuviziana kupora mifugo, kuharibu mazao, kukata miti na kuchoma nyumba
Madhara: Vifo vingi na majeruhi katika mgogoro huu unaendelea kuongezeka huku serikali na viongozi wa kanda maalum ya polisi wakipuuzia hiki kinachoendelea
Cha kushangaza sana ni kwamba sehemu inayogombaniwa ipo karibu na kambi ya jeshi na serikali inashindwa nini kupeleka wanajeshi kuweka kambi sehemu hiyo ili kuzuia mgogoro huo.
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app