DOKEZO Kuna vita ya kikoo kwa sasa inaendelea Tarime kimya kimya, baina ya koo ya Wanchari na Wakira

DOKEZO Kuna vita ya kikoo kwa sasa inaendelea Tarime kimya kimya, baina ya koo ya Wanchari na Wakira

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

huria

Member
Joined
Dec 11, 2018
Posts
35
Reaction score
93
Kuna vita ya kikoo kwa sasa inaendelea Tarime kimya kimya, baina ya koo ya Wanchari na Wakira.

Kinachogombaniwa hapa ni mashamba mipakani mwa vijiji vyao.

mgogoro huu unasababishwa na tajiri mmoja ambaye anakodisha mashamba ya koo nyingine kwa nguvu huku akidhamini vijana kutoka sehemu nyingine za tarime kupigana ili eneo hilo libaki milki yake.

Vijana wa vijiji hivi wakiwa chini ya viongozi wa kimila na koo zao wanakutana mipakani wakiwa wamejihami na mapanga, mikuki na mishale huku kila upande ukishambulia upande mwingine ana kwa ana , au kwa kuviziana kupora mifugo, kuharibu mazao, kukata miti na kuchoma nyumba

Madhara: Vifo vingi na majeruhi katika mgogoro huu unaendelea kuongezeka huku serikali na viongozi wa kanda maalum ya polisi wakipuuzia hiki kinachoendelea

Cha kushangaza sana ni kwamba sehemu inayogombaniwa ipo karibu na kambi ya jeshi na serikali inashindwa nini kupeleka wanajeshi kuweka kambi sehemu hiyo ili kuzuia mgogoro huo.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
kuna baadhi ya jamii haya mambo ya kuchinjana na kutoana uhai sio issue sana kwao. Acha sisi wa mwambao tuendelee kucheza mdundiko.
 
Kuna wakati walikuwa ni walenchoka vs wanchari...Hawa jamaa wanapenda sana vita..wangefaa sana wapelekwe kukabiliana na m23.
 
taarifa bado haijakamilika jina la tajiri anaitwa nani?

Vijiji hivyo vinaitwaje ?

Nani wachokozi wanchari au wakira?
 
Aisee hiyo vita alinisimulia babu yangu anadai ilikuwa ni noma sana
Kuna wakati walikuwa ni walenchoka vs wanchari...Hawa jamaa wanapenda sana vita..wangefaa sana wapelekwe kukabiliana na m23.
 
Back
Top Bottom