Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Kwa vile serikali ya CCM imeamua mtindo wa kubinafsisha huduma muhimu tumeona hivi karibuni wakibinafsisha shughuli za usalama kwa Majembe Auction Mart na kwa muda mrefu wamebinafsisha hata shughuli za uokoaji na kupambana na moto. Hili limekuja baada ya kubinafsisha shughuli za ulinzi wa Polisi kwa kuruhusu uwepo wa vikampuni binafsi vya polisi (private police companies).
Tumeona upungufu wa mkakati huu kwenye majanga yanayoendelea ya mvua ya Krismasi (kama nilivyodokeza, tukiwa mtandao wa kwanza kuripoti juu ya mvua hiyo masaa 12 kabla ya vyombo vya habari vya Tanzania havijarukia).
Tumeonesha kwenye suala la hospitali ya Temeke na sasa najiuliza kwenye kupambana na majanga ya moto, je serikali ya CCM itaendelea mpaka lini kubinafsisha usalama wa maisha ya watu wetu? Mpaka wapi kuungue ndio tutajua kuwa huwezi kuwa na jiji la kisasa bila ya huduma ya kisasa ya kupambana na mojawapo ya majanga ya kawaida kabisa kutokea yaani moto?
- Ilipoungua Ikulu hatukujifunza?
- Ilipoungua Benki Kuu hatukujifunza
- Ilipoungua Nasaco hatukujifunza