Hapa mnakosea. tatizo ni kuwa swali la Mzee Mwanakijiji halitoshelezi. Kinachotakiwa kuulizwa ni kuna infrastucture ya aina gani ya kupambana na moto katika jiji la Dar es Salaam? Gari la zimamoto hata siku moja halitakiwi kutegemea maji iliyoyabeba peke yake kupigana na moto. Panatakiwa kuwa na fire hydrants sehemu nyingi ili gari liweze kufyonza maji hapo. Kwenye majengo makubwa panatakiwa na njia ya maji iliyokuwa dedicated kwa ajili ya kuweza kufyonzwa panapotokea janga la moto. Zimamoto wanapokuja kwenye tukio wanatakiwa kuunganisha mipira yao hapo, yale ya kwenye gari ni ya hatua za mwanzo tu. Tulikuwa na system ya fire hydrants katika sehemu ya jiji letu na hata katika majengo lakini kama kawaida yetu tuliona ni anasa na hatukuzihudumia mpaka sasa hivi zimebakia historia. Tujiulize kuna vifaa vingapi vya kupigana na moto katika kumbi zetu za starehe, nyingi ambazo zimeezekwa na makuti? Zaidi ya hapo, ni wangapi wanajua kuvitumia ? Na jee sehemu za milango ya tahadhari ziko wazi na zinaweza kutumika? Mara nyingi milango hii utakuta imewekewe grili kwa nje ili kuzuia vibaka! Ngazi ngapi za tahadhari ziko wazi katika majengo yetu? Ni mara ngapi wafanyakazi na wanafunzi katika maofisi, mashule, hospitali wamepewa faya drill ili kuhakikisha kuwa wanajua nini cha kufanya panapotokea moto? Vituo ni nyongeza tu, ni sehemu ya infrastructure na tamaduni nzima ya kupambana na moto. Matatizo yetu ni makubwa kuliko uhaba wa vituo na vitendea kazi!
Amandla..........
Mkuu, umenikumbusha mbali. Bugando Hospital madaktari wamejengewa nyumba za mbao. Uliposema fire hiydrants nikazikumbuka kwani ziko kila jirani na nyumba ya daktari. Sijui hizo hydrants zinafanya kazi hadi leo au la.
Mwanakijiji amekumbusha kwamba hatukujifunza Ikulu ilipoungua. Binafsi nilijifunza nini Ikulu ilipoungua?
Mimi nilijifunza kwamba huduma kama fire, ambulance tayari zilishabinafsishwa rasmi hata kama haikutangazwa. Ule moto wa Ikulu haukuolewa na Fire mnayoipigia kelele. Ni kama vile mmesahau kwamba moto ule ulizimwa na Fire Section ya Knite Support.
Namba za Fire ni (022-2151885) kwa Dar na (028-2503998) pale Mwanza jIrani na Gandhi Hall. Hebu jaribu kuzipiga hata kama hakuna hatari ya moto uone utatumia muda gani kujibiwa.
Lakini jaribu Knite Support (0754-777100) au Ultimate Security (0713-123911) utafautishe response. Jaribu hata Ambulance ya Knite Support (022-2760087).
Tayari kwa mchanganuo huo tu umeshakubali kwamba Emergency Services zimeshabinafsishwa. Na muhuri wa kubinafsishwa ni pale Ikulu ilipobidi kuwaita Knite Support kuzima moto. A private company kuingiz kwenye vyumba vya ikulu kuzima moto. Unataka wabinafsishe vipi zaidi ya hapo.
Mimi nadhani tuangalie eneo jipya hili lililobinafsishwa kuliko kujadili parastatal ambayo tayari ilishakuwa marehemu.
Tusitegemee sana trainingi ya kutumia vifaa kama fire extinguisher. Sheria inatutaka hata sisi tuwe na fire extinguisher kwenye magari yetu. Unadani ni nani hapo atakuja kwako kukukumbusha jinsi ya kuitumia. Mimi ngoja niwe muwazi. Sijui kama nina uhakika kama ninaweza kuitumia ila msinicheke kwa uwazi wangu, naamini wengi mnaweza kuwa kama mimi.
Siku moja nilipinduka na gari ikabiringita mara tatu. Bahati nzuri nina mazoea ya kuendesha huku nimeweka safety-belt. Wakati gari imepinduka tairi zikawa zinaendelea kuzunguka. Mimi nikawa nahangaika kuchomokea kwenye kioo. Nilipotolewa kwa msaada wa walioshuhudia ajali wakauliza fire extinguisher iko wapi. Hata sikukumbuka kwani nilishukuru kutoka mzima.
Hivyo kwenye hatari kama hizi si rahisi kukumbuka kukimbilia fire extinguisher na hiyo panica ikiwa ni sababu ya kwanza.
Sababu ya pili ni kwamba Matumizi ya hizo extingusher ni mara chache sana kwani hakuna mtu mwenye uzoefu wa kuepukeepuka ajali hizo kiasi kwamba ikitokea basi yeye anakimbilia kwamna extinguisher. Wenye uzoefu ni hao wenye kazi yao Fire brigade.
Ni kama vile kufunga tai. Kama ofisini mwako hawalazimishi kuvaa tai basi unaweza kujikuta hujui kufunga tai siku inapohitajika.
Nimalizie hoja zangu kwa kusema kama tunataka service nzuri basi tufutewazo kwamba tuna Fire brigade tufanyie kazi kwamba tuna private fire services. Hata ambulance ukiisikia asilimia kubwa ni kwamba ni ya private hospital na si ya Muhimbili au Bugando.
Tujifunze kubadilika wakati ni huu.