Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Hahaha! NASA hawajakamata kiumbe chochote kutoka sayari nyingine, wala hawajakiona hata kimoja, kwa lugha nyingine umedanganywa mchana kweupeeeee... Hahaha! Kwenye sayari nyingine kuna viumbe ndio ila sio viumbe hai, hapa naongelea kuna vitu kama mawe, zipo nyingine zinasemekana kua na maji, kuna sayari nyingine ni almasi peke yake, madini mbalimbali kama chuma yamejaa mars, nyingine zimetengenezwa kwa gases nzito, na kadhalika, ila kiumbe hai hakijapatikana HATA KIMOJA... Anayekwambia vingine anataka kunogesha story tu.. ila ulimwengu ni mkubwa sana, sana sana ukisema uumalize utapanda rocket miaka tilioni unasafiri na bado hujafika hata nusu, kwa ukubwa huu labda siku moja tutabahatisha viumbe hai.. japo pia speed ya rocket zetu ni 11km/s, hapa hadi mars tu karibu kabisa tunatumia miezi sita kusafiri kufika... Sayari yenye maji iliyoko mbali itatuchukua miaka milioni kadhaa kwa speed hiyo hilo nalo tatizo... Tusubiri kuna technology mpya inaitwa warp drive endapo itawezekana basi tutaweza kwenda kwa sekunde tu.... Till then hakuna kitu kama uhai sehemu nyingine..
Habari za kufikirika na tekinolojia itakapokua zitakuwa habari za kufikika. Uwezo wa zana zetu hauwezi kuona detail katika galax yetu kutokana na umbali ambao mwanga tu huchukua miaka mingi kufika. Uwezekana upo ila tekinolojia tuliyonayo haina uwezo wa kufika na kubaini huko. Siri ya Mungu atakapoamua kutufunulia ndipo tutajua. Kwa sasa kaweka ukingo ambao hatuwezi kuuvuka.
Kubisha hakuna maana sana maana yake inaweza kudhoofisha juhudi za utafiti. Mbona hata dunia waliosema iko duara waliambiwa wazushi na wakauawa lakinileo hii hakuna ubishi?