Kuna vyanzo vingi vya mapato serikali ingeweza kuvibuni bila kuongeza kodi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kando ya barabara zote kunaweza kujengwa maduka yakapangishwa wamachinga. Hili linaweza kusimawa na halmamashauri za Wilaya. Majengo yakiwa ya kuvutia yatafanya mji uwe safi. Pia kujenga vyoo vya kulipia, kwa wenye maduka wataingia bure kwani kodi yao inachangia huduma za choo.

Halmashauri kujenga nyumba za kupanga, litaondoa tatizo la uhaba wa nyumba na kupunguza adha ya kuishi kwenye face me I face you. Biashara ya nyumba ni huduma pia kwa jamii na ikifanyika kwa mtaji mkubwa ina faida.

Makusanyo ya kila wilaya yanaweza kuchangia mishahara ya polisi katika Wilaya hiyo kutokana na mahitaji yake ya ulinzi. Hii itaipungizia mzigo serikali kuu. Wilaya inaweza kuajiri polisi countable wa ziada kama inawahitaji.

Kudhibiti wabadhirifu wa mali ya umma.
 
Ipeleke jukwaa la story of change. Waweza pata TZS5m. Nadhani huna haja na hela hiyo but do it for fun basi🙂
 
Simenti na nondo vitaibwa hizo nyumba zitakuwa zinaanguka na kuua wapangaji kila siku.

Labda hiyo kazi ya kujenga wapewe Wachina.
 
Nyie wazururaji si ndio mnalalamika wanawazonga sehemu za kupita kkoo, huko barabarani mtapitaje na magari yenu!
 
Utaambiwa serikali huwa haifanyi biashara
 
tujenge nchi yetu sasa. tusibweteke kwa misaada au mikopo tunayo pataka kutoka mataifa mengine.

Tafakari kwa mfano tu: hata wewe mwenyewe ikitokea unasaidiwa na mfadhali kukujengea nyumba yako ya kuishi ww na mke wako...mwanzo mwisho unadhani utakuwa huru na kujidai kama vile ungeijenga mwenyewe kwa fedha zako za kuungaunga?
basi hivi ndivyo ilivyo pia kwa nchi.

Nchi yetu itakuwa huru zaidi endapo sisi wananchi wake tutaijenga kwa kwa kulipa kodi.

Jamani Kodi ndio ndio maendeleo ya Taifa lolote lile, tusidanganyane, wala tusipige fitina kwa hili, lazima tuumie hakuna kodi laini, kodi ni kodi tu. tusijifanye masikini wa kushindwa kulipia sh 10, 50, 100, 1500 n.k. tulipe kodi
 
Hakuna serikali yoyote duniani inayo endelea bila kutoza kodi.

lazima watanzania tujenge utamaduni wa kujenga nchi yetu kwa kuchangia maendeleo.

Kama unauwezo wa kutuma pesa basi unajiweza, huwezi kusema eti ww ni masikini.

halafu unatozwa pindi unapo tuma na kutoa.

Ila kama kuna mapungufu kidogo tiyataje ili warekebishe kama inawezekana.

tulipe kodi, hakuna nchi inayoweza kujiendesha au kuleta maendeleo bila kulipa kodi.
 
Unachosema ni sawa kabisa. Ila naomba nikuulize ni sawa Zambia kms zaidi ya 1000 kununua lita moja ya petrol 1800 wakati pale kurasini nje tu ya ukuta wa bandari kituo (0-1km) raia wanunue mafuta 2500? nini manufaa ya bandari kwa raia ni yapi? Kama kodi ni muhimu kwanini wabunge nao wasilipe kodi? Hao ni raia exceptional ktk nchi hii? Unaadhani kwanini hakuna usawa huo.

Tuanzie hapo kwanza
 
Hakuna serikali yoyote duniani inayo endelea bila kutoza kodi.

lazima watanzania tujenge utamaduni wa kujenga nchi yetu kwa kuchangia maendeleo.

Kama unauwezo wa kutuma pesa basi unajiweza, huwezi kusema eti ww ni masikini.

halafu unatozwa pindi unapo tuma na kutoa.

Ila kama kuna mapungufu kidogo tiyataje ili warekebishe kama inawezekana.

tulipe kodi, hakuna nchi inayoweza kujiendesha au kuleta maendeleo bila kulipa kodi.
Hio tozo sio kodi. Ni double taxation
 
Naunga mkono hoja. Litakuwa ni jambo jema. Kwa ustawi wa jamii.
 
Pia litazalisha ajira nyingi kwa vijana. Halmashauri itapaswa kuwa na idara ya ujenzi, matatizo ya milango na madirisha mabovu ma carpenter watarekebisha. Matatizo ya maji watatumwa plumbers.

Wote hawa watalipwa mishahara kwa makusanyo ya kodi.
 
Tatizo la Serikali hii
Viongozi uwezo wao wa kubuni vyanzo vya Mapato Rafiki kwa Wananchi hawana
UKUBWA wa Serikali
DC 120
Das120
Ded200
Rc26
Ras26
Wabunge400
Mawaziri
Naibu Mawaziri
Katibumkuu
Naibu Katibu mkuu
Magari ya Gharama
Uwingi wa Wabunge
Mishahara Mikubwa ya Viongozi
Siasa CHAFU za kununua na kuhonga Wapinzani
Mishahara ya Wabunge Fake kina Halima
Mambo yote hayo Yanakula KODI
 
Kando ya barabara zote kunaweza kujengwa maduka yakapangishwa wamachinga. Hili linaweza kusimawa na halmamashauri za Wilaya. Majengo yakiwa ya kuvutia yatafanya mji uwe safi. Pia kujenga vyoo vya kulipia, kwa wenye maduka wataingia bure kwani kodi yao inachangia huduma za choo.

Halmashauri kujenga nyumba za kupanga, litaondoa tatizo la uhaba wa nyumba na kupunguza adha ya kuishi kwenye face me I face you. Biashara ya nyumba ni huduma pia kwa jamii na ikifanyika kwa mtaji mkubwa ina faida.

Makusanyo ya kila wilaya yanaweza kuchangia mishahara ya polisi katika Wilaya hiyo kutokana na mahitaji yake ya ulinzi. Hii itaipungizia mzigo serikali kuu. Wilaya inaweza kuajiri polisi countable wa ziada kama inawahitaji.

Kudhibiti wabadhirifu wa mali ya umma.
Brilliant!
 
Back
Top Bottom