Kuna wadada wema tu ila wanauza Baa, shida hizi

Kuna wadada wema tu ila wanauza Baa, shida hizi

Mkuu hata wema wana nafasi ya kuuza baa sio waivu tu. Tena huko ndiko unaweza kupata mwanamke material kwa kuwa wanajua uchungu wa maisha kuliko hawa wapuuzi na vilaza wa geti kali na waliomo kwenye ulokole. Hawa wanakuwa wametumika sana na tayari wameishajikatia tamaa ya maisha.
[emoji1666]
 
Mimi sio bro ni mwanadada. Nina umri wa kutosha sakafu ya tatu sasa.

Wewe kama ulisikiliza moyo wako na hata hukutaka kujua unaenda kuoa mtu wa aina gani mambo yakatick basi ni jambo la kushukuru Mungu lkn vipi kama mambo yangeenda tofauti? Usingeandika hiyo comment yako . Maana yangu ni kwamba angalau kabla ya kuingia kwenye mahusiano hasa ya ndoa ni better kuchukua time kujuana angalau kidogo. Neno langu sio sheria ila tusikurupuke. ahsante!
Subiri kwanza umeolewa? Na hyo miaka yako 30++
 
Ndoa zote ni game of chance, hakuna tofauti kabisa na betting.
Mambo kwenda kombo au kunyooka ni swala la bahati sana halina uhodari!! Ninachojaribu kuelezea hapa ni kwamba Kuna nafasi zinakuja mara moja tu katika maisha usipotumia akili yako haiji tena hiyo nafasi.
Kujuana kwenye mahusiano haina guarantee yoyote kama mtadumu.
Sawa rafiki.
 
Sijaolewa.
Basi kaa kimya kama huna experience yoyote ya ndoa. Me I thought umeolewa utupe ushuhuda wako maybe labda na wewe ulipitia haya ila saiv una anniversary kadhaa but uko hapa kutoa negative thoughts..

Sometimes wanawake wanafanya kazi za ajabu kama mapito tu,kwani kuna graduates wangapi wanagawa soda kwenye bm,klm,tilisho etc hao wanatofaut gan na baamed
 
Jana nilipita Baa Moja hivi usiku mkali kula, nikakuta ndio Bar inakaribia kufungwa. Ghafla nikasikia malumbano kati ya Meneja wa Baa na kabinti kamoja hivi (waitress). Kumcheki yule waitress sikuamini. Mrefu, ana rangi ya udhurungi, shape ya kwenda, pua ya kisomali halafu nywele mpaka mgongoni! Baada ya malumbano yule binti mhudumu akawa analia.

Malezi niliyopewa na wazazi wangu ni kusababisha tabasamu kwa wengine, ingawa sababu ya ziada ni uzuri wake pia, nikamuita yule waitress, nikamuuliza kulikoni mbona malumbano? Akaniambia, "kaka angu, tangu nianze kazi hapa nina siku ya 9, kila mhudumu wa kike ananichukia wanadhani nitawachukulia mabwana zao, kumbe mimi natafuta maisha".

Nikapatwa na simanzi sana. Nikamwambia basi usilie, agiza kinywaji. Akasema na kazi anaacha. Eeh! Nikashtuka, akamuuliza kaunta anamdai sh ngapi ya vinjwaji, akamlipa hela yote, akaniambia kaka angu kama unataka kuninunulia bia twende ukaninunulie kwengine ila silali na wewe, nikamwambia poa. Kumbe ananipeleka sehemu ambayo atakutana na mwenyeji wake.

Tukahama joint, tukafika kwenye night club Moja hivi, akawa anakunywa bia kwa hasira kama mtu mwenye msongo hadi nikawa namzuia, wakati tuko pale akaja dada mmoja ambaye nilimuacha primary madarasa mawili, anamuita yule waitress dada, nikamuuliza vipi mnafahamiana? Akasema huyu ni mtoto wa marehemu mama mkubwa na mimi ndio nimempokea hapa mjini anaishi kwangu, ana matatizo makubwa, na yeye ndio kanitumia msg yuko hapa ndio nimekuja, yule waitress akafurahi kuona nafahamiana na ndugu yake.

Tamaa zikanijaa, nikamuomba sana niondoke naye kwasababu mimi sio stranger kwake tena kwasababu nafahamiana na ndugu yake, akaanza kumuuliza ndugu yake mara mbilimbili kwamba unamuamini huyu kaka? Ndugu yake akamjibu ndio, namfahamu sana tangu tukiwa Primary. Ikabidi ndugu yake aniapize kwamba sitafanya ufirauni [emoji2]

Tukaondoka, nikam-drop mdg mtu kwake, nikasepa na manzi. Tumefika kwangu aisee story aliyonipa inahuzunisha sana. Aliolewa miaka 2 iliyopita na mwanaume ambaye alikuwa na familia mkoani. Yeye akiwa amaemaliza Shahada yake ya kwanza ya BAF (Bachelor of Accounts and Finance) na kazi nzuri, mwanaume akamshauri aache kazi, kwa mapenzi binti akaacha kazi. Mwaka mmoja baadaye mwanaume akaanza kumnyanyasa, na ndio akagundua kwamba mwamba alikuwa ana mke na watoto 4 mkoa X!!! Kumbe binti ni yatima na alizaliwa kwao peke yake. Anachoshukuru ni hakuzaa na yule mwanaume kwasababu mwanaume hakutaka kuzaa nae kwa wakati ule.

Nikamuuliza kwanini auze bar na taaluma yake? Akasema ilibidi akimbie ule mkoa alipoolewa aje mkoa huu kuficha aibu na kuwasahaulisha watu, na akaona hawezi kukaa tu kwa ndugu yake bila kujishughulisha na chochote wakati anatafuta ajira. Kikubwa zaidi kwenye ile bar aliyoacha kazi hakuna mtu aliyekuwa anajua binti ni msomi, alijishusha afanane nao, nikamuuliza kazi umeacha kweli? akanijibu nimeacha kaka.

Baada ya zile story usiku wa jana nikamwambia haya lala mama. Asubuhi wakati naamka nakuta kavaa pensi na t-shirt yangu vyombo vyote kaosha, nguo chafu kafua, kuna sufuria nilitakaga kuzitupa ila kaziosha zimekuwa nyeupe kama theluji. Nikamuomba anioshe vyeti softcopy, aisee ni kichwa hasa, O na A level ni vijiti tu, Sekondari zote kasoma za kike. Chuo GPA KUBWA!

Mchana nikampa maelekezo asipike nitamuagizia Chakula ikabidi sasa nimtafute yule ndugu yake akaanza ku-verify zile taarifa alizonieleza Binti. Wakuu Mimi sijaoa, il Kuna Binti ambaye nilikuwa namfikiria fikiria kumuoa ila hili ni jaribu kwakweli. Yani huu ni wakati mgumu sana napitia, sielewi kwakweli. Sijamfanya kitu tangu Jana. Sasa hivi ndio nimeingia kwangu na msosi wake wa usiku namuangalia tu hapa namna alivyotulia kwenye kochi anatazama tamthilia.
Cc: Bishop Hiluka , Ally Yakuti.
 
Basi kaa kimya kama huna experience yoyote ya ndoa. Me I thought umeolewa utupe ushuhuda wako maybe labda na wewe ulipitia haya ila saiv una anniversary kadhaa but uko hapa kutoa negative thoughts..

Sometimes wanawake wanafanya kazi za ajabu kama mapito tu,kwani kuna graduates wangapi wanagawa soda kwenye bm,klm,tilisho etc hao wanatofaut gan na baamed

Nikae kimya? Hili ni jukwaa huru mzee. Kumshauri jamaa ajipe muda kumjua huyo mwanamke hiyo ni negative thought? Yaan watu wamekutana hata week hawana basi wachukuane tu? Na inataka hadi niwe ndani ya ndoa ndio nijue ni vizuri kumjua mtu angalau kidogo kabla ya kuingia kwenye ndoa? aisee kazi ni nzito.

Haya inawezekana kwako iko hivyo ila mtoa mada yeye atachagua ushauri anaoona unamfaa.
 
Back
Top Bottom