Kuna wadada wema tu ila wanauza Baa, shida hizi

Watu wanawachukulia wahudumu wa bar kama Malaya,kama watu wasiyofaa

Hii siyo kweli

Huku nyuma Kuna maumivu makali mnoo ila Mungu ndiye anayejua
Kila field huwa akili za wahusika zinafanana hata ukiingia na tabia zako tofauti wakongwe watakuonesha mambo yanavyoenda nawe utafanana na uliowakuta. Wanacholipwa mabaamedi ni kidogo sana... kinachowawezesha kuishi ni umalaya, kuachiwa chenchi na kubambikia bill wateja.
 
Ni kweli, bar anayofanyia kazi ni platform ya kujitangaza tu lakini side hustles za umalaya ndio zinamfanya aweze kuishi, unakuta analipwa 70k kwa mwezi lakini kapanga geto, anapendeza, anakula, ana iphone jiulize anagawa vipi kipato chake.
Hakuna justification ya kufanya umalaya acha maneno yako hayo
 
huwa nawachukulia hivyo na wale wa salon za kiume. najua tu amevaa vibaya hapendi ila maisha yamemfikisha hapo. sijawahi kuacha kuwapatia walau alfu 5 ya soda wakimaliza kazi. zamani nilidhani ni ndogo nikaja gundua wakiniona wanagombania kabisa, wanajua tayari lunch siku hiyo wamepata. huwa naandaa kabisa bajeti nikitaka kwenda kunyoa. nafanya hivyo kwa upendo tu na mahubiri wanapata vilevile.
 
Hebu weka picha ya wa bar na yule unamfikiriafikiria tukupe ushauri
 
SI KILA MHUDUMU WA BAR NI MALAYA,, Kuna Bar flani kipindi npo Dom ilikua na mhudumu mzuri tu hv alikua mchangamfu sana alikua kila akiniona ananchangamkia sasa siku moja sikutaka mchezo nilimpangilia vzuri tu na nkamuahidi dau zuri tu lakn alikataa katukatu kwakua ndo walikua wanakalibia kufunga siku hyo akaniahidi nitafute siku nzuri na sehemu nyngne tupige story na anipe background ya maisha yake Aloooohh Trust me si kila mhudumu ni Malaya ni Shida tu ndo zinazowakabili na ni wachache sana wanaoshindwa kutoka kwny huo mtego..
 
Hapo ulikuwa unalengeshwa kwenye mfumo!hizo ni mbinu tu wanatumia kupata madanga ya kudumu!
 
Huyo ndg wa huyo binti ni mtu ambaye namuamini sana. Hawezi kunishuhudia uongo. Hana sababu ya kufanya hivyo. Hata Binti mwenyewe, Kwa sisi wenye macho ya rohoni anaonekana ni mkweli kabisa.
Brother take time kumstudy zaidi lakini pia katika kufanya maamuzi baadaye sikiliza dhamira yako inasemaje!
 
Dau lilikuwa dogo ila hiyo ngoma ulikuwa unaichapa.

Wengine wanapenda muanze na stori za uongo uongo kupendana ila deep down wanauza.

Msipeleke utakatifu pale hasa kwenye platform kama bar,lounge, Cassino whatever.

Mpeleke vile anavyokuja ila huyo mwamba asiweke Malaya ndani ikiwa Bado yeye si Malaya lazima alie kinyakyusa.
 
Nisiiongeze wala ku[FONT=Poppins, Monaco, Menlo, Consolas, roboto mono, andale mono, ubuntu mono, monospace]punguza kitu ila amini nakuambia, hakuna mahakama itoayo hukumu bila kukutanisha pande mbili, mshitaki na mshitakiwa na pia bado na mashahidi watahusika pia. WEWE UMEAMUA KUTOA HUKUMU KUPITIA MAELEZO YA UPANDE MMOJA KUA MAKINI SANA. HAKUNA MWENYE SHINDA AKATOA UONE RANGI ZAKE ZOTE KWA MDA MFUPI TU. NATAMAN NIKUELEZEE YALINIONISIBU KWA SCENERIO INAYOFANNA NA HIO ILA MIMI SIO MWANDISHI MZURI[/FONT]
 
Muoe mkuu usiishie kumsikitikia tu

Kama amesoma then anauza bar Kama barmaid maana yake hii elimu ya bongo ina mapungufu makubwa Sana

Anakunywa pombe anakuwa barmaid anatongozeka kirahisi inshort yupo depressed Sana

Mungu amsaidie
 
Mkubwa una roho nyepesi ila kaza ndugu yangu cha msingi usimchukue kisa ana hitaji msaada au kwa huruma ya aliyo pitia ... mchukue kwa sababu umemuelewa na unataka kuwa nae ... niseme tu fanya maamuzi kwa ubongo sio moyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…