Kuna wadada wema tu ila wanauza Baa, shida hizi

Hii story imenilumbusha miaka hiyo pale tawi la Mazimbu (SUA).
Kuna mtaa nje ya chuo pale unaitwa DARK CITY, Pana migahawa mingi ya vyakula na vyumba vya kupangisha wanafunzi wa chuo.

Sasa tulikuwa tunatoka ndani ya chuo (hostel) tunakuja kula na kurudi chuoni mimi na rafiki yangu.

Siku moja tumeingia mgahawani aisee tumekutana na mtoto mhudumu mzuurii, mweupe wastan, ana unywele wa chotara, kila mwanaume anatoa macho, kumuuliza anasema ndio ana siku nne pale toka atoke kwao kijijini huko mgeta (code).

Tukahudumiwa tukala tukamuaga tukaondoka, ile tumerud kesho kutwa yake binti hayupo, kuuliza tunaambiwa kachumbiwa na mwanafunzi mwenzetu chap. (niliumia mana nilipanga kuonja haha).


Jamaa tunamjua, kumbe kweli kamchukua kamfungia room. Kwake huko nje ya chuo alipopanga na muda mfupi kalipia mahali kaweka mtu ndani mazima mke wa mtu.

Show inaanza mwaka uliofuata wahuni wanavizia jamaa yupo darasani wanamkamua yule dada geto kwa mshikaji.

Mshikaji akaona amwemdeleze sijui kapeleka chuo cha ufundi wa nn vile sikumbuki.

Alitandkiwa mwanamke huko, akapigwa matukio ila jamaa alikuwa mpole anavumilia.

Miaka 8 baadae alishindwa akatema bungo mdomoni wakaachana.
Akaanza upya. Jamaa alikuwa anatembea njiani anaongea peke yake, full mtifuano katika ndoa yake.

Moral of the story = usikurupuke kuoa mwanamke sababu ya
1. Kuwahi wenzio wasimchukue
2. Urembo na uzuri wa usoni
3. Kabla hujasoma kwa kina na kujua tabia yake
4. Kutaka sifa ya kusifiwa mtaani, ukoo, kazini au barabaran umeoa pisi
 
Na honestly wanaume wengi wa miaka hii no 4 ndo inayowaponza mkuu. Yani ilitakiwa iwe point ya kwanza. Mara nyingi humu ukisikiliza vigezo wanavyosifia wanaume weng ni shepu na sura...wenyewe mnasema tabia mtarekebishana lakin ndo inakua inawacost wengi. Soma.kimasihara nyingi kule...weng ni demu pisi, demu mkali, etc Na naamini si kimasihara zote hupita hv, sometimes nyingne huresult katika ndoa...lakin za taabu.
 
Na yule mke mtarajiwa amfanyaje?
 
Sio wote wanaouza bar ni Malaya na sio Malaya wote ni Wauza Bar. Muuza Bar na Muhudumu wa Kempsky awana tofauti.(wote wana kutana na kuonekana na watu wengi wakiwa kazini) umalaya ni hulka ya mtu na sio mazingira au pale ulipomkuta. Nna ndugu na jamaa walio oa Wauza bar na ndoa zipo huu mwaka wa 35. Nna jamaa alio mdada anaejuza Leo hii wapo katika ndoa huu mwaka wa 22. Wapo walioa Mabinti waliosoma shule za Watawa na kulelewa na wazazi wawili walio kwenye ndoa ! Wamewaletea Waume zao HIV kwa umalaya wao uliojificha kwenye historia zao nzuri na upole wao machoni petu😭. Verify and decide.... uhenda Mungu amekukutanisha na your life partner
 
An Angalia moyo wakoo mkuu siyo kila muhudum malaya mda mwingine changamoto za maisha kama unauwezo wa kumsaidia kupata angalau kibarua msaidie usiangalie malipo yakee
 
Aiseeh kiukweli uki bahatika kumkuta bar maid mwenye shida na ndoa uka mwoa

huji kujuta Kiowa maishani mwako Wana jari Sana wanajua Nini unataka Kama mwanaume

Japo Changamoto yao ni kwenye kupima NGOMA na U.T.I nje nahayo wako vizuri Sana

na ndiyo hao wanao ongoza kwa kuwa mabibi wadogo skuhizi hakika wanajari na wabarikiwe
 
wala hawezi kuwa mlevi
 
Hakuna formula katika maisha, Inawezekana jamaa wakaja kupigwa na kuumizwa na huyo barmaid, ila pia Kuna uwezekano jamaa ndo amepata mke bora kiurahisi kabisa.
Kwa maelezo ya mtoa mada ni kama the lady ticks most of the boxes!! adimu sana mwanamke msomi kujituma kwenye shughuli za kijamii hasa usafi, hata kama ana hali mbaya kiasi gani kwenye maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…