Kuna wadadisi wanawaza kuna uwezekano Putin ni pandikizi la Marekani, ameiharibu Urusi

NATO ilishajifia.
Chizi mwingine huyu hapa, NATO ilishajifia..... wakati ndo baba lenu anawaogopa wasije kuingia Ukraine hadi kaamua kuingia vitani na Ukraine kuzuia Ukrainian kujiunga huko.

Kwahiyo unamanisha Putin wenu anaogopa wafu? Na kuwasahau Finland na Sweden ambao wanashare mpaka mrefu na tayari wamejiunga na NATO na wako mlangoni kwa Putin.
 
Wengine mnaanzisha uzi ili mpate comment,niambie baada ya kusambaratika USSR,ni chini ya kiongozi yupi Urusi,limejijenga tena na kupata heshima,tena kuwa taifa kubwa na tishio kwa ulaya nzima na marekani?"Putin apewe maua yake,tusisubiri afe".
Huna akili Urusi mafanikio iliyoyapata yalitoka West baada ya kuunganishwa kichumi, na hiyo vita USSR mafanikio aliyapata kwa kupata msaada wa jeshi la US na Ulaya ndio akajiona na kiburi lakini sasa jamaa wamempiga pini na kumnyanganya zile neema alizopata kupitia mgongo wao.,

Juzi putin amelazimika kukata mishahara ya wananchi % ili iende kusaidia vita aliyoianzisha yeye kwa ujinga wake tu sasa wananchi wake ndio wanalipa price yake matokeo yake njaa itatawala russia.

Uchumi wa Russia umeanza kuanguka hata miaka 2 ya vita haijaisha, ni suala la muda tu Urusi inaweza kua kama zimbabwe
 
Ungebakia TU huko huko Facebook [emoji1787]
 
.
 
Huyu apelekwe mirembe amechanganyikiwa.
 
Hamna kitu kama hicho mkuu
 
Nahisi aidha kwenye wapambe wake kuna mapandikizi ya Marekani waliomdanganya akaingia kwenye mkenge wa kuivamia Ukraine maana kuanzia hapo kaangukia pua mpaka basi tu, kaisambaratisha Urusi na kuirudisha mbali sana kuleeeee!!!!
 
ok,sawa mkuu...
 
Kama kuna mu USA alibatizwa na kupewa jina la Putin Kisha kuwa recruited CIA mleta mada atakuwa sawa vinginevyo itakuwa mental masturbation
 
Wajuzi wa mambo gani unahangaika sana bla bla nyingi subiri muendelee kula kipigo
 
mkuu samahani, mara nyingi huwa unaandika vitu humu ila sijawahi kuchangia,

naomba nikuulize, unaijua geografia ya majirani wa urusi pande zote?

tukianzia mashariki, technically tunaweza sema anapakana na US & Japan, kupitia upande huu wa mashariki hakuna mtu timamu atathubutu kuivamia Russia kwa sababu kwanza mpaka ni bahari, kisha misitu, milima, barafu, mapori makubwa n.k mpk ufike moscow itachukua muda mrefu mnoooo....

upande wa kusini ni maji pia, japo unaweza sema wapo turkey na jamaa wengine ambao ni former USSR, still upande huu hakuingiliki kirahisi,....

upande wa magharibi ndio yupo Ukraine, ile ni ardhi tambalale, kutoka mpaka wa ukraine mpk moscow au hata st petersburg sio mbali kihivo ukilinganisha ni njia zingine, kwaio mtu akiwa na nia ya kuivamia urusi ni lazima apite Ukraine to have any realistic chance of reaching moscow or st petersburg....., na ile ardhi ya ukraine haina milima, mabonde, wala misitu mikubwa!

ni upande huu wa magharibi ndipo wote waliojaribu kuivamia Russia waliplan kupita, kina hitler na wengineo wote waliishia either poland, na waliovuka hapo waliishia ukriane (hicho kimji cha bakmut?).......

upande wa kaskazini, kina finland licha ya kuwa na mpaka mkubwa ila hawana logistic advantage aliyonayo Ukraine, hakuna mtu ataplan kuivamia Urusi kupitia finland (tazama ramani utaelewa ninachoongea),....

kwa kuhitimisha, hapakua na namna nyingine zaidi ya hii kwa Russia, hawakua na chaguo jingine zaidi ya kuvamia ukraine,... gharama wanayolipa sasa ni ndogo ukilinganisha na gharama ambayo wangelipa endapo ukriane angeingia NATO,...... yani kuruhusu kambi za NATO luhansk na Donetsk ingekua ni hatari mnooo kwa urusi, maana wakati wowote wangeweza kumvamia na asiweze kujitetea........
 
Mei 9 imefika jamaa hajatimiza chochote, anakwenda kuhutubia, namhurumia sana huyo mzee...
Bursher Wako tu huwa hujui atakupiga ngapi sembuse mipango ya Putin ndo utaijua
 
Wengine mnaanzisha uzi ili mpate comment,niambie baada ya kusambaratika USSR,ni chini ya kiongozi yupi Urusi,limejijenga tena na kupata heshima,tena kuwa taifa kubwa na tishio kwa ulaya nzima na marekani?"Putin apewe maua yake,tusisubiri afe".
Put in
 

Palikua na namna nyingi tu ikiwemo mojawapo ya Urusi kujaribu kuishi kwa amani na majirani zake, kuacha chokochoko maana kuna matukio mengi tu ya Urusi kuvuruga vuruga majirani, wakiwemo akina Georgia. Hiyo ukraine kaivamia kuanzia kitambo tu na kuiba ardhi ya Crimea, huo ubabe na udhulumaji unasababisha majirani wasiwe na amani naye na watajiunga NATO wote kasoro akina China ambao wao ni wababe kivyao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…