Kuna wahubiri siku hizi wanauza maji, chumvi ama mafuta je walipe kodi?

Kuna wahubiri siku hizi wanauza maji, chumvi ama mafuta ili kutatua shida za watu (sina uhakika kama vinatatua).

Bei zao ni kubwa sana na wanaingiza pesa ya kutosha. Swali, Je, kuna haja walipe kodi ya mapato kwa mauzo hayo?
Wanaonunua wajengewe uelewa kuwa wanachofanyiwa sicho
 
Mwendelezo huo huo hadi kufikia kwenye kuaminishwa hapa duniani kuna wajomba zake Mungu kuliko wengine.

Yakute Goba huko uyaambie nini kuhusu Isiraeli?
watu lazima waelewe kwamba mambo matakatifu lazima yaheshimiwe.

mambo matakatifu hayakanyagwi. Hakunaga ibada ya kukanyaga mafuta matakatifu, labda mafuta ya alizeti.

hakunaga keki ya upako inashikiliwa na stiki ndio unalishwa na vipande pande vinatupwa huko jalalani. Yaan kitu kitakatifu kinatupwa hovyo hovyo, huku maji ya upako yakitumika kudeki vipande vya keki vilivyoanguka kanisani?

sasa uchafu gani unakua Mtakatifu?
huwezi kudondosha mambo matakatifu hata kidogo kama chembe ya haradali..

ni muhimu watu kuepuka ushirikina na fedheha mbele za watu 🐒
 
mimi nimeshawahi kwenda kwa Mwamposa sio mara moja wala mara mbili, udongo pale hauuzwi, kinauzwa mafuta na maji tu. na huwa anasema ukikutana na mtu akakuuzia udongo toa taarifa, pale yanuzwa mafuta na maji na ni shiling elfu moja tu kwa pc. myonge mnyongeni haki yake mpatie. ndio ni mfanya biashara ila hauzi udongo ni bure.
kumbe ni mfanya biashara eee, sasa mtumishi anakuwaje mfanya biashara? wakat yeye kama ni ufunuo wa kutumia mafuta au maji amepewa bure?? kwani yeye awauzie watu?
 
nina njaa jamani me sijui kama mfanya biashara au mtumishi niko 50G% sijui jamani sitaki dhambi
 
kumbe ni mfanya biashara eee, sasa mtumishi anakuwaje mfanya biashara? wakat yeye kama ni ufunuo wa kutumia mafuta au maji amepewa bure?? kwani yeye awauzie watu?
Yani sio tu mfanyabiashara bali ni taperi wa kitaifa na hata sarakali inajua hilo
 
Kijiko cha udongo buku.. Na kuna mtu ananunua hadi vijiko 20.. Nilishuhudia pale Kawe kwa Mwamposa mende la cbm 16 linamwaga kifusi cha udongo.. Sijui siku ile mwamposa aliingiza milion mia ngapi
Ila hii nchi sijui wajinga wataisha lini.....☹️
 
Kuna wahubiri siku hizi wanauza maji, chumvi ama mafuta ili kutatua shida za watu (sina uhakika kama vinatatua).

Bei zao ni kubwa sana na wanaingiza pesa ya kutosha. Swali, Je, kuna haja walipe kodi ya mapato kwa mauzo hayo?
Ningekua nina uwezo watu wote kama hao na wanao fanana na hao ningewaburuza mahakamani kwa tuhuma za utapeli mazee...☹️
 
Ila hii nchi sijui wajinga wataisha lini.....☹️
Asee nilikuwa najiona mjinga kipindi niko mdogo mpaka nikawa nawaza kwamba hv kwa huu uelewa wangu mdogo ntaishije hii nchi, nimekuwa nimekutana na viazi hadi najiona nina nafuu tena
 
Kuna wahubiri siku hizi wanauza maji, chumvi ama mafuta ili kutatua shida za watu (sina uhakika kama vinatatua).

Bei zao ni kubwa sana na wanaingiza pesa ya kutosha. Swali, Je, kuna haja walipe kodi ya mapato kwa mauzo hayo?
Ndio walipe maana wanafanya biashara.
 
mimi nimeshawahi kwenda kwa Mwamposa sio mara moja wala mara mbili, udongo pale hauuzwi, kinauzwa mafuta na maji tu. na huwa anasema ukikutana na mtu akakuuzia udongo toa taarifa, pale yanuzwa mafuta na maji na ni shiling elfu moja tu kwa pc. myonge mnyongeni haki yake mpatie. ndio ni mfanya biashara ila hauzi udongo ni bure.
Alipie kodi hayo mafuta na maji. Hiyo ni biashara na biashara hizo hazipo ktk Biblia.
 
Back
Top Bottom