Kuna wakati Tuseme ukweli tu,Tanzania inasonga mbele Chini ya Chama Tawala

Joined
Sep 6, 2026
Posts
58
Reaction score
44
Ukikaa chini ukatafakari Tanzania ya leo na Tanzania ya miaka iliyopita, kuna vitu vingi ambavyo huwezi kuvipuuza.

Tunaona barabara zikijengwa, madaraja yanaendelea kujengwa, vituo vya afya vinaongezeka, shule zinaboreshwa, maji yanafikishwa maeneo mbalimbali na umeme unaendelea kusambaa. Hata kwenye usafiri, kilimo na miundombinu, kuna miradi mikubwa ambayo inaendelea kufanyika.

Sasa mimi huwa nasema hivi, tusipende kulalamika tu bila kuangalia upande mwingine wa maisha. Ni kweli bado kuna changamoto, na Serikali bado ina kazi kubwa ya kufanya. Lakini pale ambapo kuna jambo zuri limefanyika, ni vizuri pia kulitambua na kulisema.

Maendeleo ya nchi hayaji kwa siku moja. Ni hatua moja baada ya nyingine. Leo tunajenga barabara, kesho tunafungua fursa za biashara, tunaboresha huduma za afya, elimu na maisha ya wananchi.

Cha muhimu ni sisi Watanzania kuendelea kuwa na uzalendo, kuvumiliana na kushirikiana. Tanzania ni yetu wote.

Tuipe Serikali nafasi ya kuendelea kufanya kazi, na pale ambapo kuna changamoto, tuseme kwa kujenga na kushauri.

๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ Tunaweza kutofautiana mawazo, lakini Tanzania yetu ibaki kuwa moja. Amani yetu ni utajiri wetu.

Kazi inaendelea. Tanzania inasonga mbele. โค๏ธ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
 
Ukiona na kuamini hivyo jua wewe ni chawa wa kunuka.
 
Tangu tupate uhuru, kasi ya maendeleo nchi hii haiendani na rasilimali tulizojaliwa kama taifa.

Maendeleo hii nchi inayopiga kwa kasi zaidi ni ufisadi wa viongozi, hawa jamaa wanafukuzana kwa utajiri.

Zunguka mikoa yote tuna madini ya kila aina, lakini tazama jamii iliyoizunguka hiyo migodi, bado hata maji safi na salama hawana uhakika wa kuyapata.
 
๐Ÿค๐Ÿ’ช
 
Hakuna amani bila haki!
 
Inasonga mbele kuelekea mautini
 
 
Kwamba vyama vingine havina uwezo wa kuongoza, sasa kwanini mnaviruhusu viwe kwenye uchaguzi.?
 

Kitu ambacho hamtaki kuelewa au mnakielewa hamtaki kukisema ni kwaba maendeleo yaliyopo hayalingani na muda na rasilimali tulizonazo. Hapa tunazungumzia miaka 65 ya Uhuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ