A
Anonymous
Guest
December 15 2025, Serikali kupitia tovuti ya makao makuu Veta ilitoa orodha ya Vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka 2026. Orodha ilibainisha jina la chuo alichochaguliwa kijana na muda wa kipindi (Asubuhi/Jioni), pia orodha ilionyesha kama ni Mwanafunzi wa bweni (Boarding) au Kutwa (Day).
Kero yangu inatoka Chuo cha Ufundi Shinyanga (Shinyanga VTC), baadhi ya Wanafunzi tuliochaguliwa bweni kama tovuti ilivyoonyesha tunaambiwa tukapange mtaani kwa madai kuwa hakuna nafasi, na mtu ukilalamika unaambiwa kama hawezi gharama za kukaa mtaani basi usitishe masomo na nafasi yako wapewe wanaoweza kumudu gharama.
Hii haijakaa sawa, mtu anatoka mikoa ya mbali mfano Mbeya, anakuja kuripoti akiwa kanunua mahitaji yote yanayohitajika kwa Mwanafunzi wa bweni halafu anafika chuoni anaambiwa akapange mtaani, hii inaleta gharama kwa wazazi ambazo hazijatarajiwa. Cha ajabu kuna wanzafunzi wapo bweni na kwenye orodha walionyeshwa kama ni wanafunzi wa kutwa.
Ufafanuzi wa Mkuu wa Wilaya, soma hapa ~ DC Mtatiro: Veta Shinyanga ina nafasi 179 za bweni lakini Wanafunzi wapo 229, nimeelekeza darasa moja liwe bweni