Ni kweli Mkuu mimi ni kijana lakini nikiwa nasikiliza hizo Vitu hivyo Vya Oliver Ng'oma wananiita mimi ni mzee 😁 kwamba ni nyimbo Za wazee!Bonge moja la mwanamziki ninaemkubali mkuu. Na hizo ngoma zote ninazo. Wapo wengine kama Mbilia Bell,Mtukuzi,Franko Makiad. Lakini kizazi hiki hawatakuelewa ukiwaambia hizo ngoma. Hata ukienda kwenye vibanda vya wachoma cd hizo ngoma hawana kabisa. Hiki kizazi ni kama hakuna watu kabisa. Yaani Bob Marley,Luck Dube hawawafahamu. Ukiwatajia kitu The Wailers unakushangaa usoni tu
Sent from my SM-C9000 using JamiiForums mobile app
Ouk sawaaahUnaweza zitafuta ukaziskiliza labda nikusaidie kidogo tafuta hizi hapa mbili kama example ili uzipe uzito kama nzuri au sio nzuri
Ng'e
Alphosine
Kama wewe ni kijana halafu umezielewa hizo ngoma,basi utaufaidi mziki mtamu. Bonge la ngoma hizo mkuu. Mimi ninaposikiliza hizo ngoma,nakuwa niko ulimwengu mwingine kabisaNi kweli Mkuu mimi ni kijana lakini nikiwa nasikiliza hizo Vitu hivyo Vya Oliver Ng'oma wananiita mimi ni mzee [emoji16] kwamba ni nyimbo Za wazee!
Oliva ngoma nyimbo zake zina ladha flani amazing, papa wemba napena ngoma yake ya "ye teho"Kuna ladha uwa nazipata sana kwenye hizo nyimbo yani fikra zangu zinarudi nyuma sana! Kuna nyimbo kama za Papa wemba ile inaitwa "Show me the way" bonge moja ya ngoma yani,
Harafu kuna ile nyingine kashirikiana na Koffi olomide "Wake up" mle wameimba aiseee