Simba ipo ngazi za juu Afrika ndani ya timu 20 bora. Nitawashangaa sana kurudi tena kwenye uswahili wa kuajiri watu aina ya Manara. Simba kwa sasa inahitaji mtu msomi na mbunifu kwenye kitengo cha habari ambaye ataikuza na kuiuza Simba mitandaoni. Simba haihitaji tena mpiga makelele au mtu wa mipasho ili kuujaza uwanja. Uwanja utajaa wenyewe kutokana na kandanda safi na matokeo uwanjani.