Kuna wanawake hawapendeki hata uwafanyie nini

Kuna wanawake hawapendeki hata uwafanyie nini

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
41,728
Reaction score
103,997
Imagine uko na mwanamke kwenye mahusiano kwa miaka 4, umemkuta Ni jobless, umepambana umemtafutia kazi yenye mshahara kila mwisho wa mwezi anapokea na posho ya elfu 10 analipwa kila siku anayofika kazini.

Mwanamke huyu umempangia
Sehemu, unamlipa Kodi januari to December miaka yote hiyo,usafir kazin na ela ya chakula kila Siku iendayo kwa Mungu unamgharamia bila kujali anapokea mshahara Wake au posho yoyote kazin kwake.

Siku unapata Safar ya mkoa wkt wa kurudi unafungasha vitu kadhaa vya jumla njiani kwa ajili ya nyumbani kwake kuanzia vitunguu, nyanya, mkaa, mchele, mahindi, viazi chips na mAfuta ya alizeti n.k yote ili kumpunguza gharama za mjini Maana uko njiani mkoani vitu umekuta vinauzwa Bei rahisi Sana.

Baada ya kuleta vitu ving nymbn unaamua kupunguza posho ya meza ya kila Siku kwa zaidi ya 50% (yaani unatoa 5,000 kwa siku) Maana tayar vitu vingi vya msingi vipo ndani, Elfu 5 iyo inakua ya kubadilishia mboga na kununulia viungo vya ziada ili kupika chakula.
 
Hujakaa Sana mjini unapata Safar nyngn tena mkoani, tena ya ghafla Sana, una mtaarifu mwenzio kua utaondoka saa flan afanye mpango muonane sehem flani kabla hujaondoka. Anasema atakuja, muda unafika hatokei na Simu zako hapokei. Unaamua kumpotezea na kuendelea na Safar zako.

Baada ya Siku 2 uko mkoani anakupigia simu njaa inauma sn Mbona umemtelekeza Siku ya pili hii hujatoa Ela yoyote ya kula.

Unamuuliza Inamaana unajisahaulisha hujui kwamba nmesafiri, isingekua njaa kukuuma inamana usingenitafuta? Anakwambia Inamaana wewe ukisafiri ndo Watu wasile? Tuma pesa hata kwa Tigo pesa nikanunue vitu vya kupika.

Unaamua kumkatia Simu na kuendelea na shughuli zako maana anatia hasira na uko anakoelekea atakukera Zaid na mtagombana, Kila akipiga Simu zake uzipokei.
 
Baadae anatumia namba ngeni unapokea kumbe ni yeye, anasema kaazima Simu ya shoga yake,mbona upokei sim zake, anaomba msamaha kwa kauli alizotoa muanze upya. Unasema sawa haina shida.

Kisha anasema vp sasa khs Ela ya kula unatuma? Unamuuliza Inamaana umeniomba msamaha ili upewe Ela ya kula au vipi? Anajibu hapana, msamaha wangu namaanisha. Unamwambia basi Kama unamaanisha jibebe mwnyw kwa Siku zilizobaki kwa mshahara na posho unazolipwa kazin kwako kila siku mpk nikisharudi.

Anadai haiwezekani kujibeba hata akiba ya Mia mbovu ndani hana,atalala njaa. Unamuuliza mshahara na posho za kazin kwake miaka 3 yote kazini anapelekaga wapi Kama anakosa hata Ela ya kujigharamia chakula kwa Siku chache hizi nilizosafiri.

Inamaana unakazi,ila Siku nisipoacha Ela ya kula wewe unakufa njaa? Anakujibu kwamba Wewe Ni mwanaume wangu, posho na mshahara wangu havikuhusu,timiza wajibu wako Kama wanaume wenzio, usitake mtelezo kupitia jasho langu.
 
Unagundua kumbe huyu mwanamke Ni mpuuzi,yaani kutumia posho au mshahara wake kujigharamia kula yake mwnyw, kwa afya Yake mwnyw, bado anaona Kama hasara kiuchumi kwake na ananitolea Maneno ya shombo hivi.

Anyway, Basi unamwambia "POA nasign out, wee njaa ikizd sn utatoa Ela yako ujinunulie chakula ule, ikishindikana kujinunulia nikirudi nikute turubai la msiba hapa nyumbani kwako, umekufa kwa njaa". Anakujibu "UTAJUA MWENYEWE, mwanaume una roho mbaya Sana wewe" unakata Simu na kuendelea na shughuli zako.

MDA Si mrefu tangu ukate Simu,
Unapokea sms za shombo akidai anajuta kukufahamu na kua na Wewe kwny mahusiano,wewe ni mwanaume mchoyo usiemjali kwa chochote kile tangu amekujua, unajali familia yako tu, hata akifa kwa njaa kwako ni sawa TU.

Inabd umpigie kutaka Ufafanuzi wa kauli ya "usiyemjali kwa chochote kile tangu amekujua" imemponyoka au Yuko serious na anachosema?. Anakujibu kwamba "ndio am serious,unadhani hivyo vi elfu tano tano vyako unavyotoa nawe utajiita mwanaume Kati ya wanaume wanaojua kupenda na kujali wanawake wao?"

Ukiwa bado unaitafakari hiyo kauli ya fedhea,anaongezea kauli nyingine ya kuudhi "Wee Kama Huwezi kunihudumia,Toa go ahead uone jins gan wanaume wenzako wanavojua kuhudumia wanawake wao". Unamjibu kwa kifupi sana "poa,Go ahead"
 
Anakwambia "kwasababu ushatoa Go ahead,Naomba namba yangu futa, nami yako nafuta na kukublock yako,kwangu usije Tena, kuanzia sahv mimi na Wewe Basi,usinizoee tena daima" unamjibu "POA" Kisha unakata Simu kuendelea na shughuli zako.

Kesho yake asbh unashangaa mtu yule yule alokwambia usimzoee na keshakublock kisa hujui kumhudumia, anakutext kukufahamisha kua anaumwa sana, hata kazin hajaenda, anaomba Ela japo ya bajaji apande aende hospitali akatibiwe atafia humu ndani, unampotezea, anakupigia sn simu zake uzipokei.

Ila ubidamu unakujia, suala la ugonjwa unalichukulia kwa uzito wake, unaamua kumpigia jiran na shoga yake wa karibu anae azima Simu yake kila Mara kukutafuta ili aende kwake afanye utafiti kisiri kujua kama anaumwa kweli serious au ni maigizo yake TU ili ujue unafanya maamuz gani.

Mrejesho shoga yake anakutext kua kamkuta mzima wa afya na wako seblen wanapiga story vzur na kakuta anakunywa bia. Ukweli unaupata na kuendelea kumchunia apambane Na maisha Yake. Upokei sim zake Wala kujibu text zake.
 
Unazoeana na shoga yake mnakua mnatext na kupigiana Simu na story za kawaida tu kujuliana Hali mara kwa Mara. Sasa Siku Moja unapokea sim ya uyo shoga ake, ghafla unaskia saut sio ya mwny simu, ni mwanamke wako mloshagombana na kuachana tayari, anajieleza kua anaomba umsikilize japo kdg ,Basi unaamua kuikata hiyo simu haraka sn. Kila akipiga Tena simu upokei.

Kumbe fursa hiyo ya kushika Simu ya shoga yake,anapata fursa nyngn ya kusoma sms zote kwny simu hiyo mlizochati na shoga Yake uyo tangu kipind icho unamtuma akampeleleze Kama anaumwa kweli au lah!.

Anakasirika na kuzua ugomvi mkubwa Sana na shoga yake uyo kua anamzunguka,kumpeleleza na kumgombanisha na bwana ake kwny mahusiano yake, Kisha anamfukuza nyumbani kwake Kama mbwa eti Ni mnafiki.

Haitoshi anaanza kukutumia sms za kashfa,matusi na dharau kua wewe Ni malaya sana, unatembea hadi na shoga zake wa karibu. Kumbe Simu zake upokei uko bize na shoga Yake mnawasiliana mnamzunguka sababu mna mahusiano ya kimapenzi mnatakana. Humjibu chochote.
 
Haitoshi pia anawapigia rafiki zako wa karibu sn kuwajulisha kua mmeshaachana sababu umemchanganya yeye na shoga Yake, Wewe ni mtu mbaya sana.

Haishii hapo anapeleka taarifa hizo kwa bwana ake na uyo shoga yake kua unatembea na mchumba wake, jamaa asivyo na ustaarabu Wala busara anakuja kichwa kichwa Bila ushahidi wowote, mtu anakuletea shutuma za kutembea na mchumba wake ila hakusikilizi Japo kidg, MDA wote anataka aongee yeye tu peke yake.

Unaona kumbe huyu jamaa nae mpuuzi, kaja kwa Shari,tayar ameshasadiki Maneno yote ya uwongo aliyolishwa uko na uyo mwanamke, hata hajui chanzo Ni nini,anakurupuka na hataki kueleweshwa.Basi mnazinguana ile mbaya liwalo na liwe. Hakuna hata kusalimiana,kila mtu kivyake.

Baada ya yote hayo alokufanyia na kukuchafua kote huko, umemkalia kimya TU, haipiti wiki anaomba tena mrudiane muanze upya,kakosea sn,yeye bado anakupenda Sana hawezi kuishi Bila Wewe.

Wakuu hivi mwanamke wa hivi unamuelewaje?[emoji848]
Screenshot_20230517-132244.jpg
Screenshot_20230517-132419.jpg
Screenshot_20230517-132507.jpg
Screenshot_20230517-132515.jpg
Screenshot_20230517-132556.jpg
Screenshot_20230517-132657.jpg
Screenshot_20230517-132707.jpg
 
🤣🤣🤣🤣

Ukweli ni kuwa mwanamke hana shida. Tatizo lipo kwako..

Ulimzoesha na mwanamke ukimzoesha inabadilika kutoka huruma kwenda sheria ya lazima.

Ila huyo ni mpumbavu, kujidai mgonjwa wakati siyo ni kujitafutia matatizo.
 
Back
Top Bottom