Naomba nichangie kufuatana na heading zaidi... Kuna ukweli mwingi kwenye kichwa cha habari ila iko hivi
Hao wanawake hawana bahati ya kuolewa ama kupata wapenzi wenye mapenzi ya kweli.. Wao huishia kutumika tu..
Kila mwanaume anayempata, mambo huwa safi kwa mwanaume hata wengine kufikia kujenga nyumba na kufanya uwekezaji
Tatizo huanza kwa mwanaume kuanza dharau na kuwa malaya sana.... Binti wa watu huishia kulia na Maumivu kisha baada ya muda hupata mwingine na kuanza upya
Huyu mwanaume haimchukui muda kugundua kuwa kapoteza mgodi hivyo hutaka kumtafuta tena mwanamke ila si kimapenzi bali kumtumia tu ili mambo yanyooke
Nina mifano hai mpaka hapa JF